Siasa Zetu : Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana wawasili Wilayani Kahama - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Friday, 5 June 2015

Siasa Zetu : Msafara wa Katibu Mkuu wa CCM Ndugu Kinana wawasili Wilayani Kahama


KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Ndugu Abdulrahman Kinana akipokelewa na kamati ya Ulinzi na Usalama usiku huu ndani ya wilaya Kahama mkoani Shinyanga tayari kwa mapumziko,ambapo kesho ataianza rasmi ziara yake katika kijiji cha Nyakanazi wilaya ya Biharamulo mkoani Kagera,Ndugu Kinana ndani ya Biharamulo atapokea taarifa za chama na Serikali na baadae kuzungumza na Wafugaji wa kanda ya Ziwa (Mikoa ya Geita,Kagera,Mwana na Shinyanga)  na baadae kueleke Bukoba mjini.

Ndugu Kinana amewasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha uhai wa chama,akiwa ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na Mbunge wa jimbo la Nzega usiku huu Dkt.Hamis Kingwangalla,mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akipokelewa na baadhi ya viongozi wa chama hicho usiku huu wilayani Nzega mkoani Tabora akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana ameambatana na Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye na baadhi ya Maofisa wa chama. 
  KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwa na baadhi ya viongozi wa chama na serikali mara baada ya kuwasili wilayani humo akielekea mkoani Kagera kwa basi maalum katika ziara yake ya kikazi ya kukagua utekelezwaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM mwaka 2010 na kuimarisha chama.Ndugu Kinana pia aliwashukuru wakazi wa wilaya hiyo kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kujenga chama na nchi kwa ujumla
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akiwashukuru wapenzi na washabiki wa chama hicho wilayani Nzega usiku huu kwa kumpokea vyema na kumtakia kheri katika safari yake ya kukijenga na kukiimarisha chama na nchi kwa ujumla
 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana akimshukuru Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla kwa mapokezi mazuri wilayani humo,ndugu Kinana amewasili wilayani humo mnamo majira saa nne usiku na ushehe akitokea jijini Dar kwa basi maalum akiwa emeambatana na ujumbe wake akielekea mkoani Kagera kwa ziara ya kikazi
 Mbunge wa Nzega Dkt Hamis Kingwangalla  akitoa ufafanuzi wa jambo kwa Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Abdulrahman Kinana .

PICHA NA MICHUZI JR.KAHAMA.

No comments:

Post a Comment