Makamau
wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali Iddi akiangalia harakati za
matengenezo ya Vitabu vya Baketi katika Kiwanda cha Uchapaji Maruhubi
wakati alipofanya ziara fupi ya Kutembelea kiwanda hicho.Kushoto ya Balozi Seif ni Kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa Serikali Bibi Hanat mohammed Aboud.
Mkuu
wa Kitengo cha Kompyuta katika Kiwanda cha uchapaji Maruhubi Nd. Moh’d
Abass Rajab akimuonyesha Balozi Seif aina za michoro tofauti
inayosarifiwa katika uchapaji wa vitabu na majarida mbali mbali
yanayopelekwa na wateja kuchapishwa kwenye kiwanda hicho.
Mfanyakazi
wa Kitengo cha Kompyuta Bibi Miza Mkiwa Jecha akimfahamisha Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Sampuli za picha na majarida
yanayotengenezwa na mashine za kisasa za Kiwanda hicho.
Nyuma
ya Balozi Seif ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Mkamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar Mh. Mohammed Aboud Mohammed na Kaimu Mkurugenzi za Uchapaji
Bibi Hanat Mohammed na Kushoto ya Balozi Seif n Katibu Mkuu Ofisi ya
Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed.
Picha na –OMPR – ZNZ.
Na Mwandishi wetu.
Serikali
ya Mapinduzi ya Zanzibar imeonya kwamba haitamvumilia mtendaji ye yote
wa Serikali au Taasisi zake za Umma atakayebainika anazorotesha ufanisi
wa kazi pamoja na kuendeleza makundi katika sehemu za kazi.
Onyo
hilo limetolewa na Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar Balozi Seif Ali
wakati akizungumza na Wafanyakazi wa Idara ya upigaji chapa na Mpiga
chapa Mkuu wa Serikali baada ya kuangalia utendaji kazi wa fanyakazi hao
katika sehemu mbali mbali za Kiwandi hicho hapo Maruhubi Nje kidogo ya
Mji wa Zanzibar.
Balozi
Seif alisema yapo mambo yanayofanywa na baadhi ya wafanyakazi wa
Taasisi za Umma ambayo hayapendezi kwa vile yanazorotesha ufanisi wa
kazi kutokana na baadhi yao kupenda majungu na uvivu wa uwajibikaji.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alionya kwamba wapo watendaji katika
Kiwanda cha Uchapaji wenye tabia ya kuendeleza uvivu jambao ambalo
linawavunja moyo wenzao walioamua kufanyakazi kwa juhudi. Hivyo
watendaji hao wanapaswa kujirekebisha mara moja.
Alifahamisha
kwamba tabia hiyo mbaya inaiumiza Serikali Kuu iliyoamua kutumia fedha
nyingi za kigeni katika kuimarisha miundo mbinu ya kisasa ya Kiwanda
hicho chenye uwezo wa kuzalisha katika kiwango chaTeknolojia ya kisasa.
“
Pamoja na changamoto zinazokukabilini katika utendaji wenu wa kazi
lakini Serikali kamwe haitosita kumchukulia hatua mtendaji ye yote
atakayeonyesha tabia ya kuanzisha makundi na uvivu katika kazi “. Alisema Balozi Seif.
Aliwaeleza
wafanyakazi hao wa Idara ya Upigaji chapa na Mpiga Chapa Mkuu wa
Serikali waelewe kwamba wanawajibika katika eneo muhimu kwa Taifa jambo
ambalo wanahitajika kuwa makini katika utekelezaji wa majukumu yao ya
kila siku.
Makamu
wa Pili wa Rais wa Zanzibar alifafanua kwamba Ofisi yake inayosimamia
Kiwanda hicho iko katika matayarisho ya kuandaa Rasimu itakayoiomba
Serikali Kuu kukifanya kiwanda hicho mabadiliko ya kuwa Mamlaka
inayojitegemea.
Alisema
hatua hiyo itasaidia kuiongezea mapato Taasisi hiyo yatakayokidhi
huduma za uendeshaji kamili pamoja na mafao ya wafanyakazi waoenbdesha
Kiwanda hicho.
Mapema
Wafanyakazi hao walielezea changamoto zinazowakabili katika utekelezaji
wa majukumu yao ya kila siku ambazo zimekuwa zikichangia kupunguza ari
yao ya kjazi.
Walisema
tatizo la usafiri kwa watendaji wanaomaliza kazi nyakati za usiku
limekuwa mtihani mkubwa wa muda mrefu, posho kwa muda wa ziada pamoja
na ukosefu wa mafunzo kweza kuzimudu vyema mashine za kisasa
wanazotumia.
Akitoa
ufafanuzi wa baadhi ya changamoto hizo Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa
Pili wa Rais wa Zanzibar Dr. Khalid Salum Mohammed alisema kwamba Wizara
hiyo itaomba ruhusa ya Serikali Kuu kununua Gari itakayosaidia
kupunguza changamoto ya usafiri kwa watendaji hao.
Dr.
Khalid alisema tatizo la posho za ziada kwa watendaji hao zimekuwa
zikilipwa na Wizara kwa mujibu wa maombi yhanavyopelekwa licha ya
kwamba Taasisi hiyo imekuwa ikitumia fedha za ziada za Idara nyengine
katika kununulia mali ghafi za kuchapisha kazi muhimu za Taasisi za
Serikali.
Akigusia
suala la mafunzo Katibu Mkuu huyo wa Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais wa
Zanzibar alieleza kuwa Wizara ina mpango wa kuwapeleka mafunzoni
wafanyakazi watano wa Kiwanda hicho kwenye kwenye mashine zinazofanana
na zile wanazotumia ili wapate uzoefu.
No comments:
Post a Comment