Mbunge wa jimbo la Arumeru Mashariki ,Joshua Nassar akishirikiana na wananchi katika kijiji cha Karangai kuweka mawe katika chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. |
Mbunge Nassar akisaidia katika hatua za awali za ujenzi wa eneo hilo. |
Mbunge Joshua Nassar akizungumza na mmoja a wanakiji cha Karangai huku akiwa amembea mtoto muda mfupi baada ya kumaliza hatua za awali za uwekaji wa mawe kwa ajili ya ujenzi wa chanzo cha maji kwa ajili ya umwagiliaji. |
Mbunge
Joshua Nassar akizungumza na baadhi ya kina mama ambao mingoni mwao
wanajishughulisha na shughuli za kilimo alipotembelea kijiji cha
Karangai kwa ajili ya hatua za awali za ujenzi wa chanzo cha maji kwa
ajili ya umagiliaji katika kijiji hicho. Na Dixon Busagaga wa kanda ya Kaskazini.
MBUNGE wa
jimbo la Arumeru Mashariki
Joshua Nassari jana ameungana na mamia ya wananchi katika kijijicha Karangai
kata ya Kikwe katika jimbo hilo kufanya shughuli za awali za ujenzi wa chanzo
kipya cha Maji kwa ajili ya umwagiliaji.
Zoezi hilo
lilo anza majira ya saa 3
asubuhi na kumalizika majira ya saa 12 jioni ilishuhudiwa Mbunge Nassari
akishiriki kazi za mikono ikiwemo kubeba mawe na kuayapanga katika eneo la mto
kwa ajili ya ujenzi wa chanzo hicho.
Akizungumza
katika eneo hilo ,Nassari
alisema lengo la ujenzi wa chanzo hicho kipya ni harakati za kuokoa mazao kwa
baadhi ya mashjamba ambayo yameanza kukauka kutokana na kukosekana kwa maji ya
kutoshja.
“Nilijitolea kulipia malori matatu kwa
siku nzima kufanya kazi hii na ununuzi wa nyaya maalum (chain link) kwa ajili
ya kufungia/kujengea Mawe kwenye eneo ambalo chanzo cha maji haya kinaanzia
lakini pia kwa sababu ilikuwa ni kazi ya kutwa nzima tulihakikisha hakuna
anayeondoka katika eneo hili hivyo tuliamua kuchinja mbuzi ,tukapika
ugali na kazi ikaendelea”alisema
Nassari.
Nassar
aliwashukuru ijana zaidi ya 300
pamoja na kina mama waliofika katika zoezi hilo kwa lengo la kuendelea kumtia
moyo.
|
No comments:
Post a Comment