Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisisitiza jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akielezea jambo wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of thanks baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Sehemu ya wajumbe wakimsikiliza Rais Jakaya Mrisho Kikwete wakati akifungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mjumbe kutoka Liberia akitoa vote of thanks baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mshereheshaji wa mkutano huo Mhe. Maria Sarungi-Tsehai akitoa maelezo baada ya Rais Jakaya Mrisho Kikwete kufungua rasmi mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkaribisha Rais Jakaya Mrisho Kikwete kupokea tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Mkurudenzi Mtendaji wa taasisi ya Twaweza Bw. Brian Eyakuze akimkabidhi Rais Jakaya Mrisho Kikwete tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akishukuru kwa kupewa tuzo maalumu ya taasisi zisizo za kiserikali kwake kwa kuwa kiongozi aliyetekeleza kwa vitendo masuala ya Serikali ya Uwazi na Ushirikiano. Hii ni wakati wa ufunguzi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete akisalimiana na Balozi wa Ujerumani nchini ambaye ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete akisalimiana na mmoja wa mabalozi ambaye ameshiriki katika mkutano huo na mabalozi wengine wengi
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete na viongozi wengine wakijiandaa kupata picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na kamati ya maandalizi mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete na viongozi wengine katika picha ya pamoja na wadau mbalimbali baada ya ufunguzi rasmi wa mkutano wa siku mbili wa Open Government Partnership (OGP) katika Ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere jijini Dar es salaam leo Mei 20, 2015
Rais Kikwete akiagana mmoja wa wajumbe wa mkutano huo. PICHA NA IKULU
HOTUBA YA RAIS DK. JAKAYA KIKWETE
Ahsanteni Sana Kwa Kunisikiliza!
HOTUBA YA RAIS DK. JAKAYA KIKWETE
Mhe.
George Mkuchika (Mb), Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais Ikulu, Utawala Bora;
Waheshimwa Mawaziri,
Katibu Mkuu Kiongozi;
Makatibu Wakuu;
Wakuu wa Taasisi za Serikali;
Wakuu wa Taasisi Zisizo za
Serikali;
Wawakilishi wa Wabia wa Maendeleo;
Wageni Waalikwa;
Mabibi na Mabwana.
Nakushukuru
Mheshimiwa George Mkuchika, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais-Utawala Bora kwa kunialika
na kunishirikisha katika ufunguzi wa Mkutano wa Pili wa Kikanda wa Washirika wa Mpango wa Uendeshaji wa Shughuli
za Serikali kwa Uwazi (Open Government
Partnership-OGP). Pia nawashukuru waandaaji wa Mkutano huu kwa kuichagua Tanzania
kuwa mwenyeji wa Mkutano wa mwaka huu. Ni heshima kubwa kwetu na kielelezo cha
imani ya washirika wenzetu wa Mpango huu kwa nchi yetu.
Kwa washiriki wote nasema
karibuni mkutanoni na nawatakia Mkutano wenye mafanikio. Wanaotoka nje ya
Tanzania nawaambia karibuni sana kwetu. Tumefurahi kuwa nanyi na bila ya shaka
wenyeji wenu watafanya kila wawezalo ukaazi wenu uwe mzuri na ushiriki wenu uwe
wa mafanikio.
Nawaomba baada ya
mkutano mtafute wasaa mkatembelee vivutio vya utalii ambavyo nchi yetu
imejaaliwa navyo. Visiwa vya marashi ya karafuu yaani Zanzibar viko mwendo wa
robo saa kwa ndege na dakika 50 kwa boti iendayo kasi. Mlima Kilimanjaro, mbuga
za wanyama za Serengeti, Ngorongoro na Ziwa Manyara na Tarangire ziko saa moja
kutoka hapa kwa ndege. Nendeni ili mrudi kwenu na kumbukumbu nzuri ya nchi yetu
na kushawishika kuja tena kwa kipindi kirefu.
Kwa namna ya kipekee
nawakaribisha wajumbe kutoka nchi za rafiki za Botswana, Nigeria, Zambia,
Uganda, Zimbabwe na Ivory Coast. Nchi zao bado si wanachama wa Mpango huu,
lakini ushiriki wao leo kama wasikilizaji ni sawa na ule msemo maarufu wa
waswahili usemao “nyota njema huonekana
asubuhi”. Bila ya shaka kuwepo kwao ni dalili njema ya uwezekano wa nchi
hizi kujiunga na Mpango huu siku za karibuni. Tunawakaribisha kwa mikono
miwili.
Nimefurahishwa sana
na uamuzi wa kutumia lugha ya Kiswahili katika sherehe hizi za ufunguzi kwa
lengo la kuwezesha umma wa Watanzania kushiriki na kufuatilia kwa urahisi kinachoendelea katika Mkutano huu. Huu ni mfano mzuri wa kutekeleza kwa vitendo
moja ya nguzo muhimu ya Mpango huu ambayo ni kushirikisha wananchi. Ni jambo muhimu
kwamba wananchi hawapati vikwazo katika kushiriki na kufuatilia mambo
yanayowahusu kwa kutumia lugha wanayoielewa. Ningefarijika sana kama mkutano
wote ungeweza kutumia lugha ya kiswahili.
Kauli
Mbiu
Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana,
Kauli mbiu ya Mkutano
huu yaani “Kuimarisha Uwajibikaji Kupitia Uwazi katika Uendeshaji wa Shughuli za
Serikali” (Enhancing Accountability Through Open Governance) ni
maridhawa kabisa. Kuendeleza uwajibikaji Serikalini ndiyo shabaha kuu ya Mpango
wa Uwazi katika Serikali. Serikali kuendesha shughuli zake kwa uwazi ni jambo
la msingi katika uwajibikaji. Wananchi ambao ndio walengwa na ndiyo sababu ya
kuwepo kwa Serikali watatambua kwa uhakika jinsi serikali yao inavyowahudumia
kama kuna uwazi. Uwazi unawawezesha watu kudai haki zao au kuwakumbusha
viongozi na watendaji Serikalini kutimiza wajibu wao kwa raia wanaotakiwa
kuwahudumia.
Kwa maneno mengine ushiriki
wa wananchi wenye tija na uwajibikaji mzuri wa Serikali ni matokeo ya
upatikanaji wa taarifa kutoka Serikalini. Taarifa hizo lazima ziwe sahihi na
zipatikane kwa urahisi na uhakika. Ili
iweze kuwa hivyo hapana budi kuwepo kwa uwazi. Taarifa huwaongezea wananchi
uwezo wa kuhoji, kufuatilia, na kuwawajibisha viongozi wao pale wasipotimiza ipasavyo
wajibu wao. Halikadhalika huwarahisishia katika mambo yanayowahusu kuchangia na
kutimiza wajibu wao kama raia wa nchi yao.
Ili Serikali na jamii
iweze kutekeleza ipasavyo dhana za uwajibikaji na uwazi italazimu kubadili
utamaduni wetu wa uendeshaji wa mambo. Hususan, tuwe na mitazamo na fikra
chanya na kuondokana na imani potofu zilizojengeka miongoni mwetu yaani Serikali,
vyama vya siasa, wananchi na asasi za kiraia kuhusu uwazi na uwajibikaji. Hali
kadhalika, inatupasa tuondokane na mitazamo kinzani baina yetu. Badala yake tunatazamiwa
kujenga madaraja ya mawasiliano, maelewano na
kuaminiana. Tunawajibika kuwa watu wamoja na wenye dhamira moja ya
kuijengea nchi yetu na kuwahudumia wananchi wake. Katu hatutakiwi kuwa mahasimu.
Ikiwa hivyo tutakuwa tumekosea sana. Tutakuwa
tumewaangusha kupita kiasi.
Dhana ya uwazi na uwajibikaji
inawahusu wadau wote yaani Serikali na asasi za kiraia ambao ndio wadau wakuu
wa OGP. Tutakuwa tunakosea sana kama tutadhani kuwa dhana hizi mbili zinaihusu
Serikali pekee. La hasha! Uwazi na uwajibikaji unazihusu pia asasi za kiraia.
Lazima nao wawe wawazi kuhusu shughuli wazifanyazo ili jamii na watu wajue
wanachokifanya kwa niaba yao, kwa ajili yao na jinsi wanavyowajibika kwao. Na
kuhusu mapato na matumizi, lazima asasi za kiraia nazo ziwe wazi kuieleza jamii
wamepata pesa kiasi gani, kutoka kwa nani, kwa ajili gani na jinsi walivyozitumia
fedha hizo? Jamii na wananchi ambao
ndiyo walengwa wa shughuli za asasi hizo wanastahili kujua kwani fedha hizo
zimetolewa kwa manufaa yao na siyo ya viongozi na watendaji wa asasi za kiraia.
Tabia ya asasi za
kiraia kukataa kuwa wa wazi na kuwa wakali wanapotakiwa kufanya hivyo siyo
sahihi. Pia ni kinyume na misingi ya Open Government Partnership. Kutokufanya
hivyo ndiko kunakozua mashaka wakati mwingine hata mizozo. Asasi za kiraia nazo
lazima ziwe wazi na zitoe taarifa za shughuli ili wananchi ambao ndiyo walengwa
waweze kujua kama kweli wamenufaika. Ili, pia, wananchi waweze kuhoji, kudai
haki na kuwataka wahusika kuwajibika. Ni vyema ikaeleweka siku hizi sehemu
kubwa ya fedha za misaada ya maendeleo hupitia asasi za kiraia hivyo
kunapokosekana uwazi kupitia utoaji wa taarifa zilizo sahihi kuna hatari ya
pesa za maendeleo ya wananchi kutokuwawafikia walengwa na kunufaisha watu
wachache. Hivyo basi, serikali inapowakumbusha kuwa wawazi na kutoa taarifa watuelewe
hivyo. Kuishutumu kuwa siyo rafiki na kuingilia asasi za kiraia si madai sahihi.
Kila anayeshiriki katika Mpango wa Open Government Partnership hana budi
kutambua kuwa anatakiwa kuwa muwazi na mkweli.
Ndiyo itikadi na falsafa kuu.
Tanzania
na OGP
Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Tanzania ni mshirika wa Mpango wa OGP na ni ya
pili kujiunga kutoka Afrika mara tu baada ya Mpango huu kuanzishwa mwaka 2011. Aidha,
ni miongoni mwa nchi nane za Afrika
(Afrika Kusini, Ghana, Liberia, Malawi,
Sierra Leone, Tunisia na Tanzania) kati ya nchi 65 duniani zilizojiunga na Mpango huu ambao ni wa hiyari. Niliamua,
kwa hiari yangu, Tanzania ijiunge katika Mpango huu kwa kutambua manufaa na umuhimu
wa kuwepo uwazi katika uendeshaji wa shughuli za Serikali. Husaidia uwajibikaji wa Serikali. Kwa kweli,
Serikali kuwajibika kwa wananchi ndiyo makusudio na uhalali wa kuwepo kwake.
Uamuzi huo ni kielelezo tosha cha utayari wangu na wa Serikali ya Tanzania kuunga
mkono kwetu dhana na falsafa ya uwazi na uwajibikaji katika kuendesha Serikali.
Kusisitiza ukweli huo, Tanzania pia ni mwanachama wa Mpango wa Afrika wa
Kujitathmini Wenyewe (APRM) na Mpango wa Uwazi katika Uvunaji wa Rasilimali
(EITI).
Ndugu Washiriki;
Mimi na wenzangu katika Serikali tumefanya
mengi kuhusu uwazi na uwajibikaji. Tumepanua na kuongeza mawanda ya uwazi
katika shughuli za serikali, demokrasia, uhuru wa wananchi kutoa maoni yao, uhuru
wa habari, haki ya kupata taarifa na ushiriki wa wananchi. Tanzania ni miongoni
mwa nchi zinazoongoza Afrika na hata pengine duniani kwa kuwa na vyombo vya
habari vingi. Hivi sasa kuna magazeti na
majarida 825, vituo vya TV 28, radio 95 ikilinganishwa na magazeti mawili,
TV moja na radio moja mwaka 1992.
Kati ya vyombo vyote hivyo Serikali ina
magazeti mawili, TV moja na radio moja. Hakuna uhakiki wa habari hivyo vyombo viko huru ingawaje
maadili ya uandishi husisitizwa na hakuna ajizi yanapokiukwa.
Tumeongeza pia, uwazi katika uendeshaji wa shughuli
za serikali. Habari hutolewa katika tovuti za Wizara na Idara husika za
Serikali kwa wote kuona. Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za
Serikali (CAG) iko wazi. Mikutano ya Bunge huonyeshwa kwenye Televisheni na kwa
mara ya kwanza wananchi wameshirikishwa moja kwa moja katika mchakato wa
kuandika upya Katiba ya nchi yetu.
Katika kutekeleza Mpango Kazi wa OGP, kama
ilivyoelezwa na Mheshimiwa Waziri wa Utawala Bora, tumekwisha tekeleza Mpango
Kazi wa Kwanza (2012/2013) na sasa tunatekeleza Mpango Kazi wa Pili
(2014-2016). Mipango kazi yote miwili imetayarishwa
kwa kushirikisha asasi za kiraia na wadau wengine. Mafanikio
yaliyopatikana katika kutekeleza Awamu ya Kwanza ya Mpango Kazi wa OGP ni
pamoja na kutoa kijarida cha Bajeti ya Serikali (Citizen’s Budget) kwa lugha nyepesi ya Kiswahili na Kiingereza kwa
ajili ya kutumiwa na wananchi wa kawaida ili waelewe vipaumbele vya bajeti ya
Serikali; kuanzishwa kwa tovuti Kuu ya Serikali inayotoa taarifa muhimu zinazoweza
kumsaidia mwananchi kupata huduma kwa urahisi; kuanzishwa kwa Tovuti ya Takwimu
Huria (Open Data), inayoainisha takwimu mbalimbali. Tovuti ya “Nifanyeje” inayoweka taarifa muhimu kuhusu
namna ya kupata huduma mbalimbali za umma imeanzishwa.
Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Utekelezaji wa Mpango
Kazi wa OGP Awamu ya Pili (2014/15 - 2015/16) umejikita katika maeneo matano
ambayo ni Utungwaji wa Sheria ya Haki ya Kupata wa Habari (Access to
Information), Uwazi katika upatikanaji wa takwimu za kibajeti, (Open Budget), Uwazi
wa matumizi ya ardhi (Land Transparency), Uwazi katika masuala ya utafutaji na uchimbaji
wa gesi, mafuta na madini (Extractive Industry Transparency) na kuanzisha
tovuti ya open data kwa kuweka
taarifa kuhusu afya, elimu na maji.
Tunaendelea
na utekelezaji wa Mpango Kazi huu na tayari tumeshapiga hatua mbalimbali.
Muswada wa Sheria wa Uhuru wa Kupata Habari tayari umeshawasilishwa Bungeni na
kusomwa kwa mara ya kwanza. Ni matumaini yetu kuwa katika vikao vinavyoendelea
kati ya sasa na Julai utakamilika. Vile vile, tunaendelea na utekelezaji wa
mambo mengine tuliyoahidi kuyapa kipaumbele. Tunauona mkutano huu kama fursa
muhimu sana ya kubadilishana uzoefu utakaotusaidia kufanya mambo yetu kwa
ufanisi zaidi. Kwa ujumla wetu
tutazungumza kwa uwazi shughuli zetu pamoja na mafanikio tunayopata na changamoto
tunazokumbana nazo katika utekelezaji wa malengo tuliyojiwekea. Aidha,
tutashauriana na kubadilishana uzoefu kuhusu kuzipatia ufumbuzi.
Ni matumaini yangu
kuwa katika Mkutano huu mtatoka na Azimio la Dar es Salaam litakalosisitiza
Uwazi, Uwajibikaji na Ushirikishwaji wa wananchi katika nchi zetu na Bara zima
la Afrika. Ni lazima tufikishe ujumbe duniani kote kuwa ni muhimu kwa Serikali
zetu kuwashirikisha wananchi na kukuza Uwazi.
Ahadi
ya Serikali
Ndugu
Washiriki;
Mabibi
na Mabwana;
Napenda
kuwahakikishia washiriki wote kuwa Tanzania itaendelea kuwa muumini wa dhati na
mwanachama asiyeyumba katika Mpango huu wa OGP. Tutaendelea kushiriki kwa kuwa
tunauona Mpango huu, na haswa dhana ya uwazi na uwajibikaji kuwa na manufaa
makubwa kwa nchi yetu na watu wake. Hatuna sababu wala dhamira ya kurudi nyuma
wala hatujutii uamuzi wetu wa kujiunga na Mpango huu, ambao kwa kweli
tumejiunga kwa hiyari yetu wenyewe. Tuko imara na tayari kuendelea na safari hii
kuelekea kwenye viwango vya juu vya uwazi na uwajibikaji. Tunafahamu safari hii
itakuwa na changamoto zake, ndogo na kubwa kwa nyakati fulani fulani wakati
wote, hata hivyo, hatutakata tama. Maadam tuna hakika na matunda mazuri huko
mbele tuendako tutasonga mbele bila ya ajizi.
Ndugu Washiriki;
Tunapoangalia nyuma
tulikotoka na hapa tulipo sasa tunayo kila sababu ya kujivunia hatua kubwa
tuliyofikia katika kuwa na taasisi na mifumo mizuri ya kiutawala na uendeshaji
zinazoakisi dhana ya uwazi na uwajibikaji. Sina budi kuwashukuru sana wadau wa
ndani yaani idara na taasisi za Serikali, Bunge, vyama vya siasa, asasi za kiraia
na vyombo vya habari kwa mchango wao mkubwa katika kujenga misingi na mifumo ya
uwazi na uwajibikaji. Hata hivyo hatuna budi kutambua kuwa safari yetu bado ni
ndefu. Hivyo hatuna budi kuongeza bidii maradufu ya sasa.
Wito wangu kwa wadau
wote na washiriki wa Mpango huu, haswa taasisi za Serikali na washirika wenzetu
wa asasi za kiraia ni kuwa tuendelee kushirikiana kwa karibu. Tufanye kila
tuwezalo na kuimarisha uhusiano na ushirikiano baina yetu. Tujenge tabia ya
kukutana mara kwa mara kuzungumzia shughuli zetu na namna ya kushirikiana. Tukifanya hivyo tutapunguza au hata kuepusha
kabisa kutokuaminiana, mizozo, migongano isiyokuwa ya lazima. Kitu kilicho muhimu kwetu ni kuwa na dhamira
ya dhati ya kutaka pawepo na maelewano na mashirikiano baina yetu. Kama hilo lipo mambo yatakuwa mazuri.
Nayasema haya
kutokana na uzoefu tulioupata katika uhusiano wetu na asasi moja kubwa ya
kiraia na kupata mafaniko makubwa. Nayo
si nyingine bali Shirikisho la Wafanyakazi ambapo mikutano yetu ya mara moja au
mbili kwa mwaka imesaidia sana kupata ufumbuzi wa masuala mbalimbali ya
wafanyakazi. Imepunguza mizozo na
misuguano, Naamini tukiwa na utaratibu kama huo na shirikisho la asasi za
kiraia mambo yatakuwa mazuri.
Hata haya ya sheria
ya Mitandao na Takwimu tukikaa pamoja yataisha tu. Kusema sheria mbaya
haisaidii, na wengine kutishia kufuta misaada haisaidii pia. Waziri mwenye
dhamana ameshasema mwenye mawazo atoe, basi pelekeni maoni. Sisi Serikali ni
wasikivu sana. Tumeshafanya mabadiliko
ya sheria nyingi tu. Ni vyema mtambue kuwa Serikali nayo inahitaji heshima
yake. Ukitaka kuonyesha ubabe nayo
itaonyesha ubabe pia. Vitisho havijengi, lakini fursa ya kuzungumza inatoa
majawabu.
Nitaangalia uwezekano wa kukutana na asasi za
kiraia kabla ya kumaliza kipindi changu cha uongozi ili tujenge utaratibu
maalum wa mazungumzo baina ya Serikali na asasi za kiraia.
Hitimisho
Ndugu Washiriki;
Mabibi na Mabwana;
Napenda kumaliza kama
nilivyoanza kwa kuwashukuru kwa uamuzi wenu wa kuchagua Tanzania kuwa mwenyeji
wa Mkutano huu muhimu. Mmetupa heshima kubwa ambayo daima tutaikumbuka na
kuienzi. Naamini nazungumza kwa niaba ya viongozi wenzangu wote Afrika pia,
kwamba tuna matumaini makubwa na Mkutano huu kwamba utazaa matunda mema yenye
manufaa kwa bara la Afrika kwa ujumla. Sisi tuko tayari kutimiza wajibu wetu,
na tunatarajia kila mdau atatimiza wajibu wake. Tukumbuke kuwa, Uwazi na
Uwajibikaji ni utamaduni, pia ni kama msumeno, unakata pande zote. “Inawezekana,
timiza wajibu wako”.
Mungu Ibariki Afrika, Mungu
Ibariki Tanzania
Ahsanteni Sana Kwa Kunisikiliza!
No comments:
Post a Comment