Matukio :Mhe. Said Mecky Sadick Afungua Maonyesho ya Dar Property Expro - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Sunday, 3 May 2015

Matukio :Mhe. Said Mecky Sadick Afungua Maonyesho ya Dar Property Expro


Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akikata utepe kufungua maonyesho ya uwekezaji katika majengo yajulikanayo kama Dar Property Expo kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015. Makampuni na mabenki mbalimb ali yanashiriki kwenye maonyesho hayo
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, wakiwapatia maelezo wananchi kuhusu namna wanavyoweza kupata nyumba na jinsi walivyowekeza kwenye majengo waliotembelea banda la Mfuko huo
Maafisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, toka kushoto, Godbless Robian, Theresia Woiso, na Augustine Paul, wakiwapatia maelezo juu ya uwekezaji katika majengo unavyoendeshwa na Mfuko huo
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Mecky Sadick, akipatiwa maelezo na Afisa wa Mfuko wa Pensheni wa PPF, anayeshughulikia uwekezaji katika majengo, Augustine K Paul, wakati Mkuu huyo wa Mkoa alipotembelea banda la Mfuko huo mara baada ya kufungua maonyesho ya siku nne ya uwekezaji katika majengo (DAR property Expo), kwenye ukumbi wa VIP wa Diamond Jubilee jijini Dar es Salaam, Jumamosi Mei 2, 2015
Wakazi wa Dar es Salaam, wakitembelea banda la PPF
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Mecky Sadick, akisikiliza kwa makini juu ya uwekezaji wa PPF katika majengo

Mkuu wa Mkoa akitembelea banda la Nevada Properties, kampuni inayojihusisha na ujenzi wa majengo
Mkuu wa mkoa akimsikilizaAfisa biashara mwandamizi wa kampuni nya Kilimani Industrial Automation Ltd, (KIAL), Shaban Issa, kuhusu mashine ya  kumnyanyua fundi ujenzi kwenda juu wakati wa ujenzi wa majengo marefu ijulikanayo kama Aerial Work Platform (AWP-Machine), wakati alipotembelea banda hilo
Meneja miko ya n yumba wa benki ya Stanbic, Bernartd Mfugale, (wapili kushoto), akimpatia maelezo ya namna ya kupata mkopo huo, Mkuu wa Mkoa Said Mdecky Sadick, alipotembelea banda hilo. Kulia ni Mercy Mosha, ambaye ni afisa wa benki hiyo
Mkuu wa mkoa akipatiwa maelezo na Mkuu wa masoko wa kampuni ya AVIC  International Real Estate (T), Ltd, Linda Zhang, wakati alipotembelea banda hilo
Mkuu wa mkoa akitembelea banda la benki ya Kenya Copmmercial Bank, (KCB), huku maafisa wa benki hiyo, EloiA. Msella, (kushoto), na mwenzake wakiwa tayari kumpatia maelezo
Mkuu wa mkoa akipatiwa maelezo na Asha Shahabu, ambaye ni afisa mahusiano na wateja, wa kampuni ya Kopa Nyumba, wakati alipotembelea banda la kampuni hiyo
Mkuu wa mkoa akisaini kitabu cha wageni cha Mfuko wa Pensheni wa PPF, kushoto ni afisa wa Mfuko huo anayeshughulikia masuala ya uwekezaji katika majengo, Godbless Robian
Mkuu wa mkoa akiangalia baadhi ya michoro ya majengo ambayo PPF tayari imewekeza kwenye maeneo mbalimbali ya nchi
Theresia Woiso, (kushoto), akimpatia maelezo mwanzanchi huyo aliyetembelea banda la PPF
Maafisa wa PPF, wakiwapatia maelezo ya kina wananchi waliotembelea banda la Mfuko huo

No comments:

Post a Comment