Matukio :Makabidhiano ya Pumpu ya Maji Kisima cha Kaburi Kikombe na Utilianaji Saini ya Mradi wa Uchimbaji Kisima Bomani Ukiwa na Thamani ya Shilingi milioni mia tatu - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Friday, 1 May 2015

demo-image

Matukio :Makabidhiano ya Pumpu ya Maji Kisima cha Kaburi Kikombe na Utilianaji Saini ya Mradi wa Uchimbaji Kisima Bomani Ukiwa na Thamani ya Shilingi milioni mia tatu


IMG_3859
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akitiliana saini ya makubaliano ya Mrai wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya Bamani na Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu
IMG_3863
 WANANCHI wa Jimbo la Kikwajuni wakishuhudia utilianaji wa saini ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa wa kisima cha Maji Safi na Salama kwa Wananchi wa jimbo hilo.
IMG_3869
MKURUGENZI wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akibadilishani Mikatabani ya makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima katika maeneo ya Bomanii Unguja Mradi huo utagharimu shilingi milioni Mia tatu, akibadilisha na Mwenyekiti wa Tanzania Youth Icon, Ndg Abdullah Miraji Othman, mradi huo utaharimu shilingi za kitanzania milioni mia tatu, utilianaji wa saini hiyo umefanyika katika Ofisi za ZAWA Mabuluu.
IMG_3889
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Zanzibar Mhe. Eng.Hamad Yussuf Masauni akizungumza wakati wa hafla hiyo ya kutiliana saini ya Makubaliano ya Mradi wa Uchimbaji wa Kisima, mradi unaosimamiwa na Tanzania Youth Icon.
IMG_3882
Waandishi wa habari wakiwa katika ukumbi wa Afisi za ZAWA Mabluu Unguja wakifuatilia makubaliano hayo.
IMG_3890
Mheshimiwa Meya ya Mji wa Zanzibar Mhe Khatib Abdurahaman Khati na Diwanj wa Kikwajuni Mhe Mahboob wakishuhudia utilianaji wa saini hiyo ya makubaliano ya Mradi wa Maji Awamu ya Pili kwa Jimbo hilo.
IMG_3897
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu akizungumza wakati wa hafla hiyo ya utilianaji wa saini ya Makubaliano ya pande hizo mbili yaliofanyika katika Afisi Kuu ya ZAWA  Mabluu Zanzibar.
IMG_3911
Waheshimiwa wakifuatilia hafla hiyo ya utilianaji wa Saini ya Mradi wa Uchimbaji wa kisima cha Maji Safi na Salama kwa Wananchi wa Jimbo la Kikwajuni, mradi huo unaosimamiwa na Tanzania Yuoth Icon na Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA)
IMG_3863

IMG_3915
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni, akimkabidhi mashine ya Pump ya Maji ya Mradi wa Kwanza wa Kisima cha Kaburi Kikombe, Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar Dk Mustafa Ali Garu,  ambao uko katika hatua za mwisho ya ufungaji wa Pump hiyo na tayari kwa kutowa huduma ya maji kwa wananchi wa Jimbo lake.
IMG_3919
Mbunge wa Jimbo la Kikwajuni Mhe Eng. Hamad Yussuf Masauni, akimkabidhi  Pump ya kuvutia maji kwa ajili ya kisima kipya cha Kaburi Kikombe, Mkurugenzi  Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk. Mustafa Ali Garu.kwa ajili ya Mradi wa Kwanza wa Uchimbaji wa Kisima cha Kaburi Kikombe ambao uko katika hatua za mwisho ya ufungaji wa Pump hiyo na tayari kwa kutowa huduma ya maji kwa wananchi wa Jimbo lake.
IMG_3926
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maji Zanzibar (ZAWA) Dk Mustafa Ali Garu, akitowa shukrani kwa Mlezi wa Jumuiya ya Tanzania Youth Icon (TAYI) kwa ushirikiano wa Taasisi hiyo na ZAWA, katika jitihada zake za kukamilisha Mradi Mkubwa wa Kisima huko Kaburi Kikobe na kutiliana saini ya makubaliano ya Mradi wa Pili wa Uchimbaji wa Kisima katika eneo la bomani Unguja ukiwa na thamani ya shilingi milioni mia tatu.

No comments:

Post a Comment

Tuwasiliane

Name

Email *

Message *

Contact Form

Name

Email *

Message *