Mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha mafuriko yaliyong'oa miti na kuharibu kingo za daraja la Kikuletwa wilayani Hai. |
Mti mkubwa ulizolewa na maji na kisha kugota katika daraja la Kikuletwa. |
Baadhi ya wakazi wa Kitongoji cha Kikuletwa wakivuka katika daraja hilo. |
Baadhi ya vijana wakiangalia namna ambayo wataweza kuondoa miti hiyo. |
Mawe pia katika barabara inayounganishwa na daraja hilo yamezolewa na maji. |
Mwenyekiti wa Kijiji cha Chmka Jacob Idd akipita katika daraja hilo kujionea athari za mafuriko hayo. |
Baadhi ya wananchi wakitizama eneo ambalo ulikuwepo mti ulisombwa na maji |
Miundo mbinu ya maji ya mradi wa Losaa Kia ambao ulikuwa unapeleka maji katika kijiji hicho ikiwa imechukuliwa na maji pia. |
Waanchi katika kijiji hicho wakijadili ni cha kufanya. |
Wakazi wa maene hayo bado wameendelea kupita katika daraja hilo kwa mashaka. Na Dixon Busagaga wa Kanda ya Kaskazini |
No comments:
Post a Comment