Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akizungumza na
waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia Maadhimisho ya Siku ya
kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa pili kushoto ni Naibu Mkurugenzi
wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi.
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuzungumzia
Maadhimisho ya Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani. Wa kwanza
kulia ni Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia
Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem wa (kwanza kulia) akiwapongeza
baadhi ya akinamama waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara
na sasa wanafanya ujasiliamali. Baadhi ya waandishi wa habari wakijitahidi kupata habari katika ukutano huo.
Mmoja wa waathiriwa wa ugonjwa wa Fistula, Lidya Makanda aliyepata
matibabu na kupona akionesha kipeperushi kilichookoa maisha yake baada
ya kukisoma na kwenda hospitali kutibiwa ugonjwa huo.
Baadhi ya madaktari wanaotoa matibabu ya ugonjwa wa Fistula katika
Hospitali ya CCBRT Tanzania wakiwa katika mkutano huo na wanahabari.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali
ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja na akinamama
waliougua fistula na kupona na kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya
ujasiliamali.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem (kulia) akihojiwa na moja ya
wanahabari mara baada ya mkutano huo.
Mwandishi wa habari wa kituo cha ITV, Sam Mahela (mwenye kipaza sauti
cha ITV) akipiga picha na akinamama waliougua fistula na kupona na
kuwezeshwa kibiashara na sasa wanafanya ujasiliamali.
Mwakilishi wa Shirika la Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya
Watu Duniani (UNFPA), Dk. Natalia Kanem na Naibu Mkurugenzi wa Hospitali
ya CCBRT Tanzania, Brenda Msangi wakipiga picha ya pamoja mara baada ya
mkutano na wanahabari katika Hospitali ya CCBRT Jijini Dar es Salaam
Na Joachim Mushi, Dar es Salaam
ZAIDI
ya akinamama 3,000 nchini Tanzania huugua ugonjwa wa fistula mara baada
ya kujifungua kila mwaka, huku sababu kubwa ya kupatwa na ugonjwa huo
ikiwa ni huduma duni za afya ya uzazi hasa zile huduma za dharura kwa
wajawazito wanapokuwa wakijifungua.
Taarifa
hiyo imetolewa leo jijini Dar es Salaam na Mwakilishi wa Shirika la
Umoja wa Mataifa linaloshughulikia Idadi ya Watu Duniani (UNFPA), Dk.
Natalia Kanem alipokuwa akizungumza na wanahabari juu ya maadhimisho ya
Siku ya kupinga ugonjwa wa Fistula Duniani.
Lakini
robotatu ya wagonjwa hao hawana uelewa wa kwamba wanaweza kupata
matibabu na kupona kabisa ugonjwa huo. Ipo haja ya kuongeza bajeti ya
huduma kwa wahusika na kutoa elimu zaidi ili kusaidia jamii hii
inayoangamia kila kukicha kwa matatizo ya fistula.
Wakinamama
na wasichana ambao hukumbwa na matatizo ya fistula wamekuwa wakipata
changamoto kubwa baada ya kutengwa na familia zao na wengine kuvunjika
ndoa zao kutokana na hali ya kuvuja mkojo muda wote huku wakitoka na
harufu kali.
Alisema
ili kuunga mkono juhudi za kukabiliana na ugonjwa wa fistula.
Hata hivyo ili kupambana na ugonjwa huo, Dk. Kanen alisema kuanzia mwaka
2003 UNFPA na wadau wenzake ilizinduwa kampeni ya dunia nzima
kuhakikisha inazuia ugonjwa wa fistula (Grobal Campaign to End Fistula)
mradi ambao kwa sasa unafanya kazi kwa zaidi ya mataifa 50 ulimwenguni
huku ukijikita kwa kuzuia, kutibu na kuwasaidia kiuchumi waathirika wa
ugonjwa huo.
Hali
hiyo imewafanya washindwe kujiendeleza katika shughuli zao za kila siku
za kujiongezea kipato, Takribani akinamama 800 wanakufa kila siku dunia
nzima kutokana na matatizo ya uzazi huku 20m kati yao wakijikuta
wameathiriwa vibaya na ugonjwa hatari wa fistula.
Inakadiliwa
kuwa kati ya akinamama 50,000 hadi 100,000 wanaosumbuliwa na ugonjwa wa
fistula ni 20,000 tu ndio hufanikiwa kupata matibabu ya ugonjwa huo kwa
mwaka.
Kwa
upande wake Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT Tanzania, Brenda
Msangi akizungumza na wanahabari kuzungumzia maadhimisho hayo yanayoanza
tarehe 23 Mwezi Mai, 2015 alisema hospitali hiyo na washirika wake
inasapoti maeneo manne ya wagonjwa wa fistula ambayo awali yalionekana
ni changamoto kwao.
Aliyataja
maeneo hayo ni pamoja na Matibabu kwa wagonjwa, Gharama za Usafiri,
Gharama za Chakula na Gharama za Malazi ili kumsaidia mgonjwa kuweza
kukabiliana na changamoto hizo.
"...Tunaomba
kila mmoja kuanzia ngazi za familia watoe elimu kwa wahusika waje
hospitalini kupata matibabu mapema kwani ugonjwa huu unatibika," alisema
Naibu Mkurugenzi wa Hospitali ya CCBRT, Brenda Msangi.
No comments:
Post a Comment