Tuzo
za watu 2015 zimetolewa Ijumaa hii kwenye hoteli ya Hyatt Regency
jijini Dar es Salaam na kushuhudiwa ‘surprises’ za kutosha. Mshindi
mkubwa kwenye usiku huo na ambaye amekuwa surprise kwa wengi ni
mtangazaji wa TBC FM, D’jaro Arungu aliyeibuka na tuzo mbili.D’Jaro
alikuwa akishindana na Millard Ayo kwenye vipengele hivyo viwili ambaye
hata hivyo alishinda pia kipengele cha blog inayopendwa.
“Mtu yeyote aliyekuwa anashindani halafu anaamini anaweza kupata nafasi lazima imshtue,” Millard ameiambia Bongo5.
“Lakini
inakushtua kwa njia nzuri kwamba kuna kitu kimemiss au labda unatakiwa
ufanyie kazi zaidi. Lakini pia kura zinamata, inachangia sehemu zote,
inawezakana ubora wa kipindi na kura pia. Lakini all in all mimi
nampongeza sana D’Jaro Arungu, ameshinda kura zote mbili, ni changamoto
pia, inatupa nafasi sisi wenyewe kushindana lakini inasaidia pia kufanya
kazi kwenye biashara yetu vizuri.”
Wema Sepetu aliyekuwa ametajwa kuwaniwa vipengele vitatu ameibuka na tuzo moja.
“I’m
Grateful… I’m humbled…. I’m out of words… Ila nawapenda for making this
happen…. Shout out to all my fans out there… Na haters pia…. I say it’s a
new beginning.”
“Therez
more to this…. I take it as a challenge and a wake up call to give you
guys more of what you want me to give,” ameandika Wema kwenye Instagram
baada ya ushindi huo,” aliongeza Wema.
Nancy Sumari akiwapongeza washindi
Hii ni orodha kamili ya washindi
Mtangazaji wa redio anayependwa
D’Jaro Arungu – TBC FM
Kipindi cha redio kinachopendwa
Papaso – TBC FM
Mtangazaji wa runinga anayependwa
Salim Kikeke – BBC Swahili
Kipindi cha runinga kinachopendwa
Mkasi – EATV
Blog/Website inayopendwa
Millardayo.com
Muongozaji wa video anayependwa
Hanscana
Muongozaji wa filamu anayependwa
Vincent ‘Ray’ Kigosi
Muigizaji wa kike wa filamu anayependwa
Wema Sepetu
Muigizaji wa kiume wa filamu anayependwa
Hemedy PHD
Hemedy PHD
Mwanamuziki wa kike anayependwa
Lady Jaydee
Mwanamuziki wa kiume anayependwa
Alikiba
Filamu inayopendwa
Kigodoro
Video ya muziki inayopendwa
Nani kama Mama – Christian Bella f/ Ommy Dimpoz
No comments:
Post a Comment