-------------------------------------------
SERIKALI
imesema itaendelea kuweka mfumo mzuri na kujenga mazingira mazuri ili
kuhakikisha biashara ya filamu inaimarika, ikiwa ni pamoja na kuwavutia
wawekezaji binafsi waliopo tayari kuwekeza katika tasnia ya filamu.
Kauli hiyo imetolewa jana jijini Dar es Salaam na mgeni rasmi wa Tuzo za
Filamu 2015, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Dk. Fenela
Mukangala alipokuwa akihutubia wakati wa hafla ya kukabidhi tuzo za
filamu.
Dk. Mukangala alipongeza juhudi za baadhi ya wafanyabiashara wa filamu
na wasambazaji ya kudhibiti uharamia wa kazi za filamu, lakini aliwataka
kuifanya kazi hiyo kwa manufaa ya wadau wote na sio kwa manufaa
binafsi.
"...Serikali
itaendelea kuhakikisha kwamba mazingira ya kufanya biashara ya filamu
yanaimarishwa. Pamoja na hayo ni vyema wasambazaji na wafanya biashara
wengine wa filamu wenye uwezo wakaepuka kulidhibiti soko la filamu kwa
nanufaa yao binafsi ili kujenga ushindani sawa," alisema Dk. Mukangala.
Aliwataka wasanii na wadau wote wa filamu kuhakikisha wanaboresha kazi
zao zaidi na kufuata vigezo vinavyotambulika ili kuzitangaza kazi zao
hata nje ya nchi.
"Napenda
mtambue kuwa ubora wa bidhaa za filamu ni moja ya vigezo vya kuwa na
soko bora la filamu, kwani filamu bora hujitangaza zenyewe. Tuhakikishe
kuwa tunaongeza weledi na ubunifu. Hivi ndivyo vigezo vilivyoifanya
sekta ya filamu nchi zilizoendelea kufika hapo ilipo," aslisema Waziri
Dk. Mukangala.
Kwa
upande wake, Rais wa Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFA), Simon
Mwakifwamba aliiomba serikali kuangalia uwezekano wa kujenga chuo
maalumu kwa ajili ya filamu ili kuijengea uwezo zaidi tasnia kwani ina
mchango mkubwa katika kuzalisha nafasi za ajira kwa makundi anuai.
Waliojishindia
tuzo za filamu kwa mwaka huu 'Tanzania Film Awards 2015 (TAFA)' katika
vipengele mbalimbali ni pamoja na Irine Sanga (Best Screen Play), Hissan
Muya (Best Actor Supporting Role), Grace Mapunda Best Actress
Supporting Role), Amri Athuman-King Majuto (Best Comedian), Irene Paul
(Best Actress), John Kalage (Best Director) na wengineo.a
Tuzo za filamu nchini ‘Tanzania Film Awards’ 2015 (TAFA).
Tuzo
hizi kubwa ambazo zimefanyika kwa mara ya kwanza jijini Dar es Salaam
katika Ukumbi wa Mwalimu Nyerere International Conference Center.
Zimewezeshwa na Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, TRA,
EATV na EAR, International Eye Hospital, Foreplan Clinic, R&R
Associates, Simu Tv na Barazani Production.
No comments:
Post a Comment