Ofisa Mtendaji Mkuu wa TTCL, Dkt Kamugisha Kazaura (kulia) akizungumza
na Waziri wa Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof. Makame Mbarawa.
KAMPUNI
ya Simu Tanzania (TTCL) leo imesaini mkataba na Mfuko wa Mawasiliano
kwa Wote (UCSAF) wenye gharama ya USD 2,244,376/- milioni (sawa na Tsh
4.1/- bilioni) kwa ajili ya kupeleka mawasiliano ya simu katika kata 19,
yenye vijiji 76.
Kata
hizo zinatakazonufaika na mradi huu ni pamoja na; Gelai Meirugoi, Arash
na Olbalbal- Arusha, Mbondo - Lindi, Makame Shambarai na Masieda-
Manyara. Kata nyingine ni pamoja na Ivuna - Mbeya, Masagati na Mombo-
Morogoro, Vikumbulu- Pwani, Ligera. kwa upande wa Mkoa wa Ruvuma zipo
kata ya Lukumbule, Marumba, Nakapanya na Nampungu. Aidha kwa mkoa wa
Singida zipo kata za Minyughe na Urughu, mwisho kata ya Ubangaa iliyopo
mkoa wa Tanga.
Mkataba
ambao leo unasainiwa rasmi, Kampuni ya Simu Tanzania (TTCL) itatoa
huduma za kawaida za mawasiliano ya simu yaani maongezi na huduma za
ujumbe mfupi (SMS) na Intaneti.
Mradi
huu utakapokamilika, utaleta chachu ya ukuaji wa wa maendeleo katika
kata hizo ikiwa ni pamoja na; wananchi wataweza kuwasiliana na pande
zote za dunia, kupata na kutumia taarifa za kibiashara, kupata habari za
masoko mapya na za kijamii.
Aidha,
huduma hii itawawezesha kutoa fursa sawa na watu wa maeneo ya mijini
ili kuendelea kujenga uwiano sawa wa kupata na kutoa taarifa kwa
maendeleo ya jamii.
No comments:
Post a Comment