Texas
Black Belts club Seminar , imeandaliwa na Sensei Ramon Veras, Dan 7,
Okinawa Goju Ryu Kyokai, mjini Houston, Texas tarehe 19 April, 2015. Pia
ni sehemu moja ya maandalizi na marekebisho ya mbinu na ufundi wa
vipande tofauti katika mfumo mzima wa Sanaa na tayari kwa baadhi ya
washiriki kwa msafara wa kwenda kwenye chimbuko la Karate huko Okinawa,
Japan.
Sensei Rumadha Fundi, ni mmoja ya wawakilishi wa Goju Ryu Jundokan, atayoiwakilisha Tanzania kwenye msafara huo..
Baada
ya takriban miaka 23 sasa, sensei Rumadha Fundi “Romi”, anarejea tena
chini Japan kama alivyofanya mwezi May mwaka 1992. Safari hiyo ya mwezi
June kwenda Naha City, Okinawa kwa njia ya Los Angeles, Tokyo na
hatimaye Naha City, Okinawa.
Sensei
Rumadha amepewa mwaliko kama mwakilishi wa Jundokan Tanzania, kwa niaba
ya kuwa mteule na mwakilishi wa chama hicho cha mtindo wa Okinawa Goju
Ryu, chini ya rais wake ambaye ni mtoto wa Eiichi Miyazato mwanzilishi
wa chama hicho Sensei Yoshihiro Miyazato “Kancho”, na hatimae kupewa
jukumu la kusambaza Jundokan nchini kote akiwa“Tanzania Chief
Instructor ” na kupewa madaraka ya kutowa idhini na mikanda ya
wawakilishi wa Jundokan nchini Tanzania na utambulisho wa kutowa vyeti (
Dan Certificate) kutoka, Naha, Okinawa.
Sensei
Rumadha anashikilia Dan 6 toka Tanzania Karate-do Federation, na Dan 3
toka Jundokan Kyokai.Lengo na madhumuni ya sensei Rumadha ni kusambaza
ufanisi wa Goju Ryu na mbinu za “Muchimi” ni undani halisi wa utumiaji
mbinu kifasaha na kitamaduni kama ifanyavyo huko Okinawa, Japan.
Sensei
Rumadha, atafanya mazoezi katika dojo ambayo mwalimu wake yeye Sensei
Bomani na Master Morio Higaonna walikuwa wanafunzi hapo miaka 45-50
iliyopita. Pia Sensei Rumadha, atatembelea sehemu zenye historia ya
mwanzao wa Karate na makaburi ya waanzilishi wa Sanaa na makumbusho ya
Karate na vitongoji vyake kama, Naha, Shuri na Tomari, Okinawa , Japan.
Nia na
madhumuni makubwa ni kutaka kuiendeleza Goju Ryu Karate Tanzania na
hatimae kuwa na walimu wenye utambulisho huko, Okinawa, Japan na kuleta
maendeleo na maslahi ya kimaisha kama mwalimu wa Karate.
Pia
Sensei Rumadha alisema “ Tapenda kubadilisha mfumo wa jinsi Goju Ryu
inafundishwa Tanzania. Tawapa mwaliko wanafunzi wote wenye nia ya
mafanikio na utambulisho toka Okinawa, kuwa chini ya uongozi wangu na
kuendeleza utamaduni wa Goju Ryu. Goju Ryu ina matawi mengi na uongozi
tofauti, mimi napendelea kuwa na shina la Okinawa Goju Ryu Karate – do,
lililowekwa na waanzilishi wa mtindo huo; lengo ni kuwa na Goju Ryu
halisi na sio mabadiliko”, alisema Sensei Rumaha..
CHOJUN MIYAGI ( Goju Ryu Karate )
Mwanzilishi
wa mtindo wa Okinawa Goju Ryu Master Chojun Miyagi , mzaliwa wa
Higashimachi, Naha, Okinawa April 25, 1888. Miyagi alianza mafunzo ya
karate akiwa na umri wa miaka tisa (9), chini ya Ryuko Aragaki, ambaye
alimtambulisha kwa Kanryo Higashionna (Higaonna Kanryo) wakati
alipofikisha umri wa miaka 14.
Mafunzoni China.
Mwezi
May 1915, kabla ya kifo cha Kanryo Higashionna, Chojun Miyagi alikwenda
jimbo la Fujian, huko China. Alipokuwa China, Miyagi aliweza kutembelea
kaburi la mwalimu aliyemfundisha mwalimu wake Karyo Higashionna aitwae
RyuRyu Ko. Baada ya kifo cha mwalimu wake Karyo Higashionna, October,
1955, Miyagi alifanya safari yake ya pili China, huko Foochow. Pia
inaaminika kwamba, muda aliyokuwa huko China, Master Miyagi, alijifunza
Shaolin na Pakua Chuan huko Fuzhou Shaolin Temple. Hapo ndipo kwa mara
ya kwanza, master Miyagi alipopata kuona mbinu za mikono mitupu (
Rokkishu) yenye msisitizo wa kinga za duara ya kiganja na ngumi zenye
mfano wa Kata, na muonekano wa kijihami nakinga na mashambulizi. Hapo
ndipo alipotunga “Tensho kata” toka katika misingi ya Sanaa ya Shaolin.
Kutoka
katika mchanganiyiko wa mtindo wa Naha –te (Mkono wa Naha), akaanzaisha
mtindo mpya kabisa. Japo ya kuwa ni mtindo mpya bila ya jina, alichukua
muda hadi mwaka 1929 ambapo Miyagi akaipa jina Sanaa ya mtindo wake
“Goju-Ryu” akimaanisha “ Ngumu na Laini”.
Kurudi Japan
Baada
ya miaka mingi huko Chini, Miyagi alirudi mjini Naha na kufungua shule
au dojo.Alifundisha kwa miaka mingi na kuwa maarufu katika kisiwa cha
Okinawa, na hata bara, Japan. Mtindo wa Goju Ryu, ni mtindo wa kwanza
kutambulika na shirikisho la Sanaa za kujihami la Japan, “Dai Nippon
Butokukai ”. Alitambulisha Karate katika jeshi la polisi wa Okinawa,
shule za sekondari na jamii zote. Akatunga kata ya Sanchin, ambayo ina
maana ya hali ngumu ya tafsiri ya Goju Ryu, pia akatunga Tensho kata
kama upande wa laini wa Goju Ryu Karate.
Hizi
kata zina maadilifu ya jinsi na namna Miyagi alikuwa na nia kufundisha
mtindo wa ngumu na laini. Na moja ya hizo change moto ni mfano wa kata
ya juu na mwisho za Goju Ryu, inayoitwa “ Suparinpei “ inaundani wote wa
tabia na mwenendo wa Goju Ryu. Pia Miyagi, alikuwa anaipenda sana kata
iitwayo “ Shisochin “. Kata ya Tensho, inamaadili mengi toka kwa ndege
aitwae “ White Crane kata ,”Ryokushu ”. Pia Miyagi alitunga kata za
msingi kama vile, “ Gekisai Dai Ichi, Gekisai Dai Ni ” mwaka 1940.
Alitumia mbinu nyingi toka katika kata ya Suparinpei na kuongeza kata
zingine kama vile, “ Sanchin &Saifa “ambazo ni za ngazi ya juu pia.
Kifo na Historia
Baada
ya kifo chake Octoba, mwaka 1953, wanafunzi wa ngazi ya juu wa Master
Miyagi kwa wakati huo ni; Seko Higa, Eiichi Miyazato (Mwanzilishi wa
Jundokan dojo), Meitoku Yagi ( mwanzilishi wa Meibukan Dojo) ambae
alipokea sare au uniform na mkanda wa Master Miyagi toka katika familia
ya Miyagi, Seikichi Toguchi (mwanzilishi wa Shorei - Kan Goju Ryu), na
kwa upande wa bara ya Japan Gogen Yamaguchi (mwanzilishi wa
International Karate-do Goju Kai) baada ya kujifunza kwa Miyagi,
aliteuliwa kama mwakilishi wa Goju Ryu bara la Japan mbali na visiwa
vya Okinawa.
EIICHI MIYAZATO ( mwanzilishi wa Jundokan dojo)
Master
Eiichi Miyazato, alijiunga na Ryukyu ( Okinawa) polisi kwa ushauri wa
Master Miyagi mwaka 1946. Alikuwa anafundisha chuo cha polisi kama
msaidizi wa Master Miyagi ambaye alikuwa anafundisha jeshi la polisi la
Okinawa. Eiichi Miyazato, alikuwa anafundisha Judo pia. Baada ya kifo
cha Master Miyagi 1953, Miyazato, alirithi vifaa na vitu vyote alivyo
wacha Master Miyagi, hata uniform (Gi) na mkanda (obi) toka kwa familia
ya Miyagi. Hapo ndipo alipo anza kufundisha dojo iliyowachwa na master
Miyagi itwayo “ Garden Dojo “.
Mwaka 1970 aliteuliwa kama makamu rais wa “ Okinawa Judo Federation” na “ Okinawa Prefecture Karate-Do Federation”.
Tarehe
20 mwezi March, 1988, Okinawa Goju –Ryu Karate- do Kyokai, ilimuenzi
na Dan ya 10 ya Karate na pia kupewa Dan ya 7 ya Judo toka “Kodokan”,
na kuwa rais wa
Okinawa Judo Federation “ wakati huo.
Master
Eiichi Miyazato alifariki mwezi wa disemba, mwaka 1999, Naha ,
Okinawa. Juu ya kifo chake, Kodokan ilimuenzi na Dan ya 8 ya Judo. Wengi
wa wanafunzi wa Eiichi Miyazato ni pamoja na ;
Chuck Merriman, Nanko Minei, Keikichi Nakasone, Kenei Shiabuku, Masaji Taira, Koei
Teruya, Ronald Yamanaka, Tony Foster and Tetsunosuke Yasuda. Miyazato's dojo is now run by his son, Yoshihiro Miyazato.
Riyosei Arakai, Shinzo Chinen, Teruo Chinen, Yoshio Hichiya, Morio
Higaonna, Koshin Ihan, Shinichi Iribe, Masanari Kikukawa, Seikichi
Kinjo, Tetsui Gima, Tsuneo Kinjo, Atsumi Lida, Kenei Shimabukuro,
Hiroshi Ganaha, Kazuya Higa, Hisao Sunahawa, Richard Barrett, Mike
Clarke, Chuck Merriman, Nanko Minei, Kekiichi Nakasone, Kenei Shiabuku,
Masaji Taira, Koei Teruya, Ronald Yamanaka, Tony Foster, Testunosuke
Yasuda, Ryoichi Onaga, Masataka Muramatsu, na Sensei Nantambu Camara
Bomani ( Mwanzilishi wa Hekalu la kujilinda; Jundokan Tanzania), ni
mwalimu wa kwanza kutoa wanafunzi watano wenye ngazi ya mkanda mweusi
mwaka 1976 ni; Zebedayo Mapfumo Gamanya, Tola Sodoinde Malunga, Daudi
Magoma Nyamuko Sarya, Abome Mabruki na Adombe Mabruki. Sensei Bomani
alikuwa ni mwafunzi wa Eiichi Miyazato toka 1968 hadi kifo chake 1999.
Hao wote ni walimu wa kuu duniani wa Jundokan Karate duniani na kupitia
mafunzo chini ya Eiichi Miyazato sensei.
No comments:
Post a Comment