VIONGOZI wa Serikali
ya Mkoa wa kusini Pemba wakiongozwa na mkuu wa mkoa huo Mhe:Mwanajuma Majid
Abdalla na Mkuu wa Wilaya ya Mkaoni Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, wakizungumza na
mbunge wa jimbo la Mkanyageni Habibu Mnyaa wakati walipokuwa wakivuka kuelekea
kisiwa Panza kwa lengo la kuwafariji wananchi waliopatwa na maafa ya nyumba zao
kuezuliwa na upepe.
MIONGONI mwa nyumba
zilizokumbwa na maafa kufuatia upepo mkali uliovuma usiku wa kuamia Aprili 22
mwaka huu, huko katika kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani, upepo huo ulizikomba bati
zote katika nyumba hiyo
WANANCHI mbali mbali
wakiangalia nyumba iliyoangua hasa kufuatia upepo mkali uliovuma katika kisiwa
Panza Wilaya ya Mkoani, Usiku wa Kuamkia Aprili 22 mwaka huu
MIONGONI mwa nyumba
zilizokubwa na maafa kufuatia upepo mkali uliovuma usiku wa kuamia Aprili 22
mwaka huu, huko katika kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani, upepo huo ulizikomba bati
zote katika nyumba hiyo
MKUU wa Mkoa wa
Kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla akiangalia nyumba ilikubwa na maafa
baada ya upepo mkali kuezua bati zote, huko Kisiwa Panza Wilaya ya Mkoani kulia
ni Mkuu wa Wilaya hiyo Mhe:Hemed Suleiman Abdalla.
MUEMBE ukiwa umengolewa na Upepo mkali uliovuma katika kijiji
cha kisiwa Panza, ambapo uliweza kumwangukia ngombe ambaye alikuwa amefunga
maeneo hayo na ngombe huyo kuchinjwa
SHEHA
wa Shehia ya
Kisiwa Panza Chumu Abdalla Abdalla, akiwaonyesha viongozi wa Serikali ya
Mkoa wa kusini Pemba, Miti aina ya Mikoko iliyoharibiwa vikali na
upepo huo ulioleta
athari kwa wananchi wa kisiwa Panza
JENGO la madrasa
ambalo ukuta wake umeanguka chini na paa lake kuezuliwa baada ya upepo mkali
uliovuma kisiwa Panza na kusababisha maafa kwa wananchi wa kisiwa hicho
MKUU wa Mkoa wa
kusini Pemba Mhe:Mwanajuma Majid Abdalla, akiwafariji wananchi waliopatwa na
maafa ya nyumba zao kuezuliwa mapaa na upepo mkali uliovuma kisiwani humo
MKUU wa Wilaya ya
Mkoani Mhe:Hemed Suleiman Abdalla, akizungumza na wananchi wa kisiwa Panza mara
baada ya kuwafariji wananchi wao waliopatwa na maafa ya nyumba zao kuezuliwa
mapaa na upepo mkali ulivuma kisiwani humo
No comments:
Post a Comment