Kaimu
Mkurugenzi wa Masoko na Mauzo wa Shirika la Nyumba la Taifa Tuntufye
Mwambusi na Meneja wa Uendelezaji Biashara wa NHC, Willia Genya
wakibadiliashana mawazo katika hafla hiyo.
Mchechu
akibadilishana mawazo na watendaji wa DSE wakati wa utiaji saini
makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi katika mradi wa
kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es Salaam. Ujenzi
wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa unaendelea.
Mkurugenzi wa Hazina na Uendelezaji Biashara wa Shirika la Nyumba la
Taifa, David Misonge Shambwe akiwakaribisha wageni katika hafla hiyo.
..............................................................................................
Kwa
mara nyingine Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) leo Jumatano, 22 Aprili
2015 tumefikia makubaliano rasmi ya mauzo ya sehemu ya eneo la ofisi
katika mradi wa kipekee mpya wa Morocco Square, Kinondoni Jijini Dar es
Salaam. Ujenzi wa mradi huo wenye huduma mbalimbali za kisasa
unaendelea.
Mkataba
unaosainiwa leo baina ya pande hizi mbili utagharimu kiasi cha dola za
kimarekani 1,800,000 (bila VAT) kiasi cha shilingi za kitanzania 3.366
bilioni malipo yatakayofanyika kwa awamu nne katika kipindi cha miaka
mitatu.
Mradi
wa kipee na wa kwanza Tanzania wa Morocco Square wenye ukubwa wa mita
za mraba 105,000 unaotarajia kukamilika ndani ya kipindi cha Miaka
Mitatu, ni unaotekelezwa kwa kutumia mfumo mpya kabisa wa ujenzi wa
(Design and Building).
Umebuniwa
kwa makini kabisa kulingana na mahitaji ya majengo ya sasa na ya baadae
na vile vile unajengwa na mkandarasi wa kitanzania. Sambamba na haya,
utekelezaji wa mradi huu umezingatia uwepo wa huduma zote muhimu
sambamba na miundo mbadala yakujitosheleza.
Sifa
nyingine za ziada za mradi huu ni pamoja na uwepo wa majengo pacha
mawili makubwa ya ghorofa, moja likiwa na ghorofa 17 na 19.
Jengo
hili limebiniwa likiwa na mahitaji muhimu yakiwa sehemu moja (Mixed
Development) ikiwepo maeneo maalum ya Maofisi ya kimataifa, Sehemu ya
hotel kwa ajili ya wafanyabiashara, nyumba za makazi (Residential
apartment), maeneo ya maegesho ya magari, huduma za kibenki, pamoja na
sehemu ya huduma za masoko ( shopping mall).
Mradi
huu unatarajiwa kuboresha mazingira ya biashara katika jiji la Dar Es
Salaam vile vile ukizingatia mahitaji ya ukuaji na upanukaji wa jiji la
Dar Es Salaam. Jengo la Morocco Square lipo karibu kabisa na kitovu cha
jiji likiwa limezungukwa na maofisi na makazi muhimu kabisa.
Eneo
la Morocco Square linatoa fursa kwa mkazi kuweza kufika kwa karibu
kabisa sehemu mbalimbali muhimu za jiji la Dar Es Salaam kama vile
Mikocheni, Oystebay, Masaki,Mikocheni, katikati ya jiji la Dar Es
Salaam,Kinondoni, Kawe na Mlimani City.
Makubaliano
haya kati ya Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) pamoja na Soko la Hisa la
Dar Es Salaam ( Dar Es Salaam Stock Exchange (DSE) yanatoa fursa za
kipekee kwa (DSE) pamoja na mawakala wake wa soko la mitaji na tunapenda
kulipongeza soko la hisa kwa kuwahi kabla ya mashirika yote ili kuweza
kupata fursa ya kipekee katika jengo hili la kisasa kabisa na la kwanza
Tanzania.
Tunapenda
kutoa wito kwa Mashirika ya kimataifa, yakati ( Medium Enterprises)
kuchanmkia fursa hii ya kipekee ususani ukizingatia kwamba miji yote
Duniani soko la hisa huwa chachu ya maendeleo ya wadau wote wanaofanya
biashara kuzunguka eneo husika.
Sifa
za ziada za mradi huu ni kuwa na eneo maalumu linalowezesha kutua
helikopta, eneo kubwa la maegesho ya magari ya ziada, Ofisi ya Meneja wa
Usimamizi wa Milki, eneo maalumu la kukusanyia taka, nyumba ya mlinzi,
umeme wa uhakika, miundombinu ya zimamoto, mfumo wa vipoza joto, kebo za
mtandao wa mawasiliano, lifti, ulinzi wa saa 24 wa Kamera za CCTV na
kisima kirefu cha maji chenye mfumo wa kusukuma maji ya kutosha.
Tunawahamasisha
wenye kuhitaji maeneo ya ofisi, biashara na nyumba za kuishi wafanye
mawasiliano na Makao Makuu ya Shirika na kukamilisha taratibu mapema kwa
ajili ya kuweza kuingia kwenye mchakato ulio wazi wa manunuzi.
Ukiwa
mdau na mnunuzi mtarajiwa, ama una ndugu/rafiki anayetamani kununua
ofisi au kuwekeza katika mradi huu, tafadhali wasiliana na Kitengo cha
Mauzo, Makao Makuu ya NHC au piga simu namba 0754 444 333; baruapepe: sales@nhctz.com na pia tembelea tovuti ya Shirika www.nhctz.com kwa maelezo zaidi.
No comments:
Post a Comment