Maisha Yetu :NexLaw Advocates Watembelea Vituo viwili vya Kulelea Watoto Yatima, jijini Dar es salaam - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 10 April 2015

Maisha Yetu :NexLaw Advocates Watembelea Vituo viwili vya Kulelea Watoto Yatima, jijini Dar es salaam

 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates chini ya jengo  la PPF TOWER (Zilipo ofisi za kampuni hiyo) wakipakia vitu kwenye gari kabla ya kuanza safari kuelekea Vituo viwili vya kulelea watoto ambavyo ni House of Blue Hope kilichopo Mabibo na Msimbazi Children’s Home vilivyopo jijini Dar es Salaam.
  Baadhi ya Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakimsikiliza Bwana Daudi Mboma muanzilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima  cha  House of Blue Hope kilichopo Mabibo Jijini Dar es salaam.
 Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakimsikiliza Bwana Daudi Mboma ( hayupo pichani) muanzilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima  cha  House of Blue Hope kilichopo Mabibo Jijini Dar es salaam.
 Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakiwa kwenye picha  ya pamoja na watoto na Bw. Daudi Mboma (katikati mwenye t shirt ya mistari mistari) ambaye ni mwanzilishi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha House of Blue Hope kilichopo Mabibo pamoja na watoto wanaolelewa kituoni hapo. 
 Dr. Saudin Mwakaje pamoja na Wakili Stanley Mabiti wakikabidhi moja ya zawadi kwa mwanzilishi wa kituo cha House of Blue Hope Bw. Daudi Mboma kilichopo Mabibo Dar es Salaam.
 Partners wa NexLaw Advocates wakijadili jambo baada ya kuwasili katika kituo cha kulelea watoto cha Msimbazi Childrens Home
 Mr. Nuhu Mkumbukwa mmoja wa partners wa NexLaw Advocates akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s home.
 Sister Anna Francis, mlezi wa kituo cha kulelea watoto cha msimbazi Childrens Home akiwa amembeba mmoja wa watoto wanaolelewa katika kituo hicho.
 Nexlaw Advocates waliandaa chakula cha mchana kwa ajili ya kula pamoja na wafanyakazi wa Msimbazi Children’s Home.
 Wafanyakazi wa Msimbazi Childrens Home Centre wakichukua  chakula.
 Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakipata chakula cha mchana pamoja na wafanyakazi wa Msimbazi Children’s Home Centre.
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam
 Baadhi ya wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakielekea kukabidhi bidhaa zilizopelekwa Msimbazi Children’s Home  Centre cha Msimbazi jijini Dar es salaam
 Sister Anna Francis mlezi wa kituo cha watoto cha Msimbazi Children’s Home wakijadili jambo na wafanyakazi wa NexLaw Advocates.

Wafanyakazi wa NexLaw Advocates wakiwa kwenye picha ya pamoja kabla ya kuanza safari ya kuelekea vituo  vya kulelea watoto ambavyo ni House of Blue Hope kilichopo Mabibo na Msimbazi Childrens Home kilichopo Msimbazi Center vyote vya jijini Dar es Salaam.

No comments:

Post a Comment