Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki akizungumza na watendaji ,
waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa mkoa wa Dar es salaam wakati
akizindua Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na
watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
Mkuu
wa Wilaya ya Temeke, Sophia Mjema akizungumza na watendaji , waganga
wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es salaam kueleza nafasi yake katika
kusimamia utekelezaji wa wakati Mpango Kazi wa kuharakisha kupunguza
vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka 5 kwa mkoa wa Dar es
salaam.
Mganga
Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe akiwasilisha mpango
Kazi wa Kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama, Watoto wachanga na
watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mkoa wa Dar es salaam.
Baadhi
ya watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa wilaya na mkoa wa Dar es
salaam waliohudhuria uzinduzi wa Mpango kazi wa Kupunguza Vifo vya akina
mama wajawazito na Watoto chini ya miaka 5 wakimsikiliza Mkuu wa
mkoa huo Mhe. Sadiki Meck Sadiki (hayupo pichani) Picha/Aron Msigwa.
Na. Aron Msigwa – MAELEZO.
Mkuu
wa Mkoa wa Dar es salaam, Saidi Meck Sadiki amezindua Mpango Kazi wa
kuharakisha kupunguza vifo vya akina mama na watoto walio chini ya miaka
5 kwa mkoa wa Dar es salaam na kukemea tabia ya baadhi ya watumishi
wasio waadilifu wanaotumia lugha za kuudhi, kejeli na vitendo vya
unyanyasaji kwa akina mama wajawazito wanaofika kupata huduma za uzazi
katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati.
Akizungumza
katika kikao kilichowahusisha watendaji wa mkoa , waganga wakuu wa
wilaya na mkoa wa Dar es salaam leo jijini Dar es salaam, Mhe. Sadiki
amesema watumishi wa afya wa mkoa huo wanao wajibu wa kutekeleza
majukumu yao na kutimiza malengo yaliyowekwa na Serikali ya kuwapatia
huduma bora za afya akina mama wajawazito na watoto walio na umri chini
ya miaka 5 yaliyowekwa na mkoa.
Amesema
kuwa katika kutekeleza mpango kazi huo Serikali haitasita kuwachukulia
hatua za kinidhamu na kisheria watumishi wa afya watakaobainika
kushiriki katika vitendo ubadhirifu na wale watakaosababisha kwa namna
moja au nyingine vifo vya mama wajawazito na watoto chini ya miaka 5
watakaofika hospitalini kupata huduma za afya na kupoteza maisha yao
kutokana na uzembe wa watumishi katika vituo husika.
Amebainisha
kuwa mkoa Dar es salaam pamoja na mambo mengine umeweka mikakati
mbalimbali ya kuhakikisha kuwa inawafikia akina mama na watoto na
kuwapatia huduma bora akina mama wajawazito wanaofika katika vituo vya
afya vya Serikali kupata huduma za uzazi ili kukabiliana na vifo vya
akina mama na watoto vinavyotokea.
Ameeleza
kuwa Tanzania imekuwa ikitekeleza malengo ya millennia (MDG)ambayo
yalipangwa kukamilika ifikapo Desemba 2015 na kuongeza kuwa katika
utekelezaji wa malengo hayo bado inakabiliwa na changamoto za kupunguza
vifo vya wajawazito ambavyo amesema kwa takwimu za mwaka 2013
zinaonyesha vifo 410 kwa kila vizazi hai 100,000.
“
Tanzania katika jambo hili tumepiga hatua japo bado tunakabiliwa na
changamoto ya kuendelea kupunguza vifo hivyo kufikia 133 kwa kila vizazi
hai 100 if ikapo mwezi Desemba 2015”
Amesema
akiwa kiongozi wa mkoa huo atahakikisha lengo hilo linatimiza kabla ya
muda uliopangwa na kuwataka watendaji wa afya kwa ngazi zote kutimiza
wajibu wao ipasavyo na kuzitumia rasilimali zilizopangwa kutekeleza
malengo yaliyopangwa ili kuhakikisha kuwa vifo vinavyotokana na uzazi na
vile vya watoto wachanga vinapungua .
“Nachoweza
kusema, uwezo wa kukabiliana na changamoto hii tunao tukiunganisha
nguvu zetu kwa mazingira tuliyonayo ya taasisi za Serikali na Binafsi
bado tunayo nafasi nzuri ya kutimiza malengo yaliyowekwa, kwa sasa
tunaendelea na mkakati wetu wa kuongeza wodi za kujifungulia akina mama
wajazito wilaya ya Temeke, Ilala na Kinondoni ili kuongeza wigo wa
huduma za afya” Amesemaa.
Ametoa
wito kwa wataalamu wa afya kuendelea kutoa elimu ya afya ya uzazi kwa
akina mama wajawazito ili waweze kuelewa umuhimu wa kuhudhuria Kliniki
kabla na baada ya kujifungua za afya kupitia mpango wa TIKA
utakaoanzishwa katika jiji la Dar es salaam utakaowawezesha kupata
huduma za afya kwa mwaka mzima kwa gharama nafuu.
Katika
hatua nyingine Mhe. Sadiki amewataka wakurugenzi wa manispaa za Dar es
salaam kuendelea kutenga fedha kwa ajili ya motisha kwa watumishi wa
afya wanaotumia muda mwingi kazini wakiwahudumia wagonjwa hususani akina
mama wachanga na watoto chini ya miaka 5 wa mkoa huo.
Kwa
upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Dkt. Grace Maghembe
awali akiwasilisha Mpango Kaziwa Kuharakisha kupunguza vifo vya akina
mama, Watoto wachanga na watoto walio chini ya umri wa miaka 5 kwa mkoa
wa Dar es salaam amesema kuwa licha ya kuwepo kwa changamoto
mbalimbali toka kuzinduliwa kwake miaka 2 iliyopita na Rais Jakaya
Kikwete umepata mafanikio.
Amesema
kuwa pamoja na kuongezeka wa idadi ya wazazi wanaojifungua kutoka
97,807 hadi 134,838 mwaka 2012 hadi 2014 vifo vya uzazi vimepungua
kutoka 123 hadi 99 katika vizazi hai 100,000.
Amesema
mafanikio zaidi ya huduma ya afya ya mama na mtoto katika mkoa wa Dar
es salaam bado yanakabiliwa na changamoto mbalimbali zikiwemo kiwango
kidogo cha matumizi ya huduma ya uzazi wa mpango wa asilimia 47, kiwango
kidogo cha asilimia 51 ya wajawazito wanaohudhuria Kliniki angalau mara
4 chini ya lengo kitaifa ambalo ni asilimia 90.
Aidha
ameeleza kuwa mkoa unaendelea kuchukua hatu mbalimbali za kuhakikisha
kuwa huduma ya afya ya mama na mtoto inaimarika katika jiji la Dar es
salaam kwa kuiweka huduma hii kuwa kipaumbele cha mkoa na kuongeza
usimamizi shirikishi wa huduma za afya, mafunzo kazini kwa watumishi,
kuongeza vitendea kazi, dawa na vifaa tiba pamoja na kuhamasisha
ushiriki wa wadau na wafadhili mbalimbali.
No comments:
Post a Comment