Watani wa jadi, miamba ya soka Afrika Mashariki na kati Simba Sports club na Young Africans SC kwa
dakika chache leo baadae katika uwanja wa taifa jijini Dar, wataweka
upinzani wao pembeni watakapoungana na mamilioni ya waTanzania na dunia nzima kwa ujumla kupinga mauaji ya ndugu zetu albino, pale watakapovaa fulana zenye maneno IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO mara watakapoingia uwanjani kupasha viungo moto (Warm up) Siku ya leo kabla ya mchezo huo unaotarajiwa kuwa mkali kuanza.
Balozi Henri Mdimu |
Wakiongea kwa nyakati tofauti Mwenyekiti wa kamati ya IMETOSHA Bw Masoud Kipanya na Balozi wa kujitolea wa harakati ya Imetosha mwandishi wa habari maarufu Henry Mdimu
ambaye ni mlemavu wa ngozi (albino) waliueleza mtandao huu kuwa jana
kutwa walikuwa wakimaliza taratibu za kuwasiliana na vilabu husika yaani
Simba na Yanga pamoja na shirikisho la soka nchini TFF ili kuweka mambo sawa ambapo timu hizo pamoja na waamuzi wote watavalia fulana zenye maneno IMETOSHA MAUAJI YA ALBINO, imeelezwa
kuwa kila timu itavaa rangi zake za asili ambapo Yanga itavaa fulana za
njano zenye maandishi ya kijani na Simba sc watavaa fulana nyeupe
zenye maandishi mekundu wakati
waamuzi watavaa fulana nyeusi zenye maandishi meupe. Mchezo huo wa ligi
kuu ya vodacom unatarjiwa kuchezwa kesho jioni katika uwanja wa Taifa
jijini.
Mwandishi wa habari hii amevipongeza vilabu hivyo vikongwe nchini Simba na Yanga kwa kuweka upinzani wao pembeni na kuungana na mamilioni ya waTanzania nchi nzima akiwemo Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mh J.M Kikwete kupinga
vikali kabisa mauaji manyanyaso na udhalilishwaji wa jamii hiyo ya
albino, aidha alipongeza shirikisho la soka nchini TFF kwa kuwezesha
jambo hili adhimu kufanyika.
"MUNGU TUBARIKI TANZANIA"
Toka kushoto Mkala Fundikira(Mjumbe) Henry Mdimu(Balozi) Masoud Kipanya( Mwenyekiti) na Kelvina John( Mjumbe) |
No comments:
Post a Comment