TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Rais ateua Mwanasheria Mkuu wa Serikali mpya
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho
Kikwete amemteua Bwana George Mcheche Masaju kuwa Mwanasheria Mkuu wa
Serikali.
Uteuzi wa Bwana Masaju
ulianza jana, Ijumaa, Januari 2, 2015 na ataapishwa keshokutwa,
Jumatatu, Januari 5, 2015, Ikulu, Dar Es Salaam.Kabla ya uteuzi wake,
Bwana Masaju alikuwa Naibu Mwanasheria Mkuu wa Serikali. Bwana Masaju
pia amepata kuwa Mshauri wa Sheria wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu,
DAR ES SALAAM.
3 Januari, 2015
No comments:
Post a Comment