MKATABA
wa kujenga tena umoja na kukiunganisha upya Chama Tawala cha Sudan Kusini cha Sudan People’s Liberation Movement (SPLM)
ulitiwa saini usiku wa jana, Jumatano, Januari 21, 2015, katika sherehe ya
kufana iliyofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Hoteli ya Ngurdoto, Wilaya ya
Arumeru, Mkoa wa Arusha.
Mkataba
huo unaojulikana kama Agreement on the Re-unification of Sudan
People’s Liberation Movement umepongezwa kuwa ni hatua muhimu katika
kulitoa taifa changa la Sudan Kusini katika hali ya machafuko, vita vya wenyewe
kwa wenyewe, kutoelewana na kutoaminiana, mambo ambayo yameligubika taifa hilo
tokea mwishoni mwa 2013 wakati kutokuelewana kulipozuka ndani ya SPLM na
hatimaye katika Serikali ya nchi hiyo.
Viongozi
waliotia saini ni Mheshimiwa Salva Kiir Mayardit, Rais wa Sudan Kusini ambaye
pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa
Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia aliyekuwa Makamu
wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO)
na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Sherehe
hiyo ilishuhudiwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya
Mrisho Kikwete ambaye pia ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho
ndicho kimesimamia mazungumzo yaliyozaa Mkataba huo. Rais Kikwete pia ndiye
mdhamini mkuu wa Mkataba huo.
Wengine
walioshuhudia tukio hilo muhimu ni Rais wa Uganda, Mheshimiwa Jenerali Yoweri
Kaguta Museveni; Rais Uhuru Muigai Kenyatta wa Kenya; Naibu wa Rais wa Jamhuri ya
Afrika Kusini Mheshimiwa Cyril Ramaphosa, Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM
Mheshimiwa John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo
yaliyozaa Mkataba huo na Katibu Mkuu wa CCM Mheshimiwa Abdulrahman Kinana
ambaye alikuwa mwezeshaji wa mazungumzo.
Mazungumzo
yaliyozaa Mkataba huo yalianza mwishoni mwa mwaka jana baada ya Rais Kikwete na
Chama cha CCM kuombwa na Rais Kiir Mayardit kukubali chama hicho tawala cha
Tanzania kutumia uzoefu na ujuzi wake wa miaka mingi wa uongozi na siasa
kujaribu kuleta suluhu ndani ya SPLM.
Mazungumzo
hayo ya kutafuta suluhu ambayo yamefanyika kwa awamu mbili, ya kwanza yakiwa
yamefanyika Oktoba mwaka jana na pili yakiwa yameanza mwanzoni mwa mwezi huu,
Januari 2015, yameongeza thamani kwenye
mazungumzo mengine yanayofanyika Addis Ababa, Ethiopia chini ya usimamizi wa
taasisi ya IGAD na yanayojadili jinsi ya kurejesha amani nchini humo.
Viongozi
wa SPLM wanaamini kuwa kwa sababu mgogoro wa kisiasa nchini mwao ulianzia ndani
ya chama hicho na kwa sababu SPLM ndicho chombo pekee ambacho kinawaunganisha
wananchi wote wa Sudan Kusini, basi busara inaelekeza kuwa suluhu ianze kutafutwa
ndani ya chama hicho.
Mkataba
wa jana, kimsingi, unalenga kuweka mazingira ya kujenga utulivu, maelewano, amani
na umoja wa kudumu ndani ya chama hicho na nchini humo kwa kuhakikisha kuwa
utekelezaji wa mambo ya msingi yaliyokubaliwa kuhusu shughuli za siasa, uongozi
na oganisheni ya chama hicho yanafanyika bila kukawia.
Mkataba
huo pia unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinabuni na kutekeleza sera za
kuondokana na ukabila, makundi yenye mitazamo finyu na mwenendo wa kijeshi
katika siasa za Sudan Kusini.
Aidha,
Mkataba huo unalenga kuhakikisha kuwa chama cha SPLM kinafanya mageuzi ya
kuanza kujenga utamaduni wa kuvumiliana na ujenzi wa misingi ya demokrasia.
Mkataba
huo pia unataka watu wote ambao walishiriki katika mauaji na umwagaji damu
katika vita vya wenyewe kwa wenyewe wasiruhusiwe kugombea wala kushika nafasi
ya uongozi wa umma ndani ya chama hicho.
Pia
viongozi wote wa Sudan Kusini wanatakiwa, chini ya Mkataba huo, kuwaomba radhi
wananchi wa nchi hiyo ya Sudan Kusini kwa kuruhusu nchi hiyo kuingia katika
machafuko ya umwagaji damu mkubwa.
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
– Dar es Salaam.
22 Januari,2015
Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Mhe Bernard Membe akikaribisha viongozi na wajumbe katika mkutano huo
Waziri Mkuu Mstaafu na Makamu Mwenyekiti wa zamani wa CCM Mheshimiwa
John Samwel Malecela ambaye ndiye alikuwa mwenyekiti wa mazungumzo yaliyozaa
Mkataba huo akisoma muhtasari wa mazungumzo hayo
Sehemu ya ukumbi wa mkutano huo
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiongoza utiaji wa saini wa Mhe. Salva Kiir Mayardit Rais wa Sudan Kusini ambaye pia ni Mwenyekiti wa SPLM na anayeongoza kundi linalojulikana kama SPLM in Government (SPLM-IG), Mheshimiwa
Dkt. Riek Machar ambaye alikuwa Makamu Mwenyekiti wa SPLM na pia
aliyekuwa Makamu wa Rais wa Sudan Kusini anayeongoza kundi la SPLM in Opposition (SPLM-IO) na Dkt. Deng Alor Kuol ambaye anaongoza kundi la SPLM Leaders- Former Detainees (SPLM Leaders – FD).
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akiwa na Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol wakionesha hati baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akitoa pongezi kwa Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto), Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) na Bw. Deng Alor Kuol
baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na
kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na
kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Yoweri Museveni wa Uganda akiongea
Dkt. Riek Machar akiongea
Rais Uhuru Kenyatta wa Kenya akiongea
Rais Jakaya Mrisho Kikwete, Naibu Rais wa Afrika Kusini Cyril Ramaphosa (kulia) na Bw. Bw. Deng Alor Kuol wakifurahia wakati Rais Salva Kiir Mayardiy wa Sudan ya Kusini (wa pili kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini
Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa
Sudan Dkt Riek Machar Teny (wa pili kulia) wakipeana mikono
na kubadilishana nyaraka baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano
ya kukiunganisha upya chama cha SPLM cha Sudani Kusini katika hoteli ya Ngurdoto jijini Arusha Jumatano Januari 21, 2015 usiku.
Rais Kikwete na Bw. Dkt Kuol wakipiga makofi wakati Rais Salva Kiir Mayardit wa Sudan ya Kusini (kushoto) na Makamu wa Rais wa zamani wa Sudan Dkt Riek Machar Teny wakipeana mikono kwa furaha baada ya kutia saini mkatana wa makubaliano ya kukiunganisha
Naibu Rais wa Afrika ya Kusini Mhe Cyril Ramaphosa akiongea na kupongeza hatua iliyofikiwa
Rais Kikwete akiongea na viongozi na wajumbe katika mkutano huo. Picha na IKULU
No comments:
Post a Comment