BBC inazindua tuzo kwa heshima na kumbukumbu ya mtangazaji wake Komla
Dumor, mwaka mmoja baada ya kufariki dunia ghafla mwaka jana akiwa na
umri wa miaka 41. Komla Dumor alikuwa mtangazaji wa aina yake, ambaye
katika maisha yake aligusa wengi- si nchini mwake Ghana pekee bali pia
Afrika na duniani kote. Alionesha taswira ya Afrika katika ujasiriamali,
ubashasha na kujiamini. Kupitia
uandishi wake wa habari wa kusisimua na usimulizi wake, Komla alifanya
kila awezalo kuinadi Afrika, ulimwenguni.
BBC inakusudia kuendeleza hiba ya Komla.
BBC inatangaza kuanzisha tuzo ya "BBC World News Komla Dumor Award".
Tuzo hiyo itatolewa kwa mwandishi wa habari anayefanya kazi na kuishi Afrika, ambaye ataonesha ujuzi na ubunifu wa hali ya juu katika uandishi wa habari na jinsi anavyoandika habari na taarifa za Afrika, na ambaye ana nia na ari ya kuwa mwandishi nyota wa habari.
Kupitia tuzo hiyo, BBC inawekeza katika mustakbali wa uandishi wa habari wa Afrika, kwa kumpa nafasi mshindi ya kwenda BBC na kuonesha habari na taarifa za Afrika duniani kote.
Mshindi pia atapata nafasi ya kupata uzoefu zaidi kwa kufanya kazi na idara mbalimbali za BBC katika kipindi cha miezi mitatu atakachokuwa London. Mshindi huyo vilevile atapewa nafasi ya kutangaza katika TV, radio na hata kwenye tovuti na kuwafikia wasikilizaji, wasomaji na watazamaji wapatao milioni 265 duniani kote.
Kufahamu zaidi jinsi ya kuwania tuzo hiyo, bonyeza link hii:
http:// careerssearch.bbc.co.uk/ jobs/job/komladumoraward/ 10717

http://
No comments:
Post a Comment