Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifanya ziara ya ukaguzi kwenye
machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.
Muu wa
Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa (kushoto) akikaga vifaa vinavyotumika
kwenye uchinjaji mifugo na uandaji wa nyama kwenye machinjio ya Kisasa
Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akikagua utunzaji wa nyama kwenye
chumba maalumu cha kutunzia nyama zinazosubiri kusafirishwa kwenye
machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9, 2015.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akifanya majumuisho ya ziara yake
ya ukaguzi kwenye machinjio ya Kisasa Kizota Mjini Dodoma Januari 9,
2015, wengine ni wafanyakazi wa machinjio hiyo.
Mkuu
wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Chiku Gallawa akiwa kwenye picha ya pamoja na
wafanyakazi wa machinjio ya Kisasa Kizota mara baada ya kufanya ziara ya
ukaguzi kwenye machinjio hayo Januari 9, 2015.
Alitoa
agizo hilo mwishoni mwa wiki (Jan 9,2015) alipofanya ziara ya ukaguzi
kwenye Machinjio hiyo ya kisasa iliyopo Kizota Mjini Dodoma
inayomilikiwa na kuedeshwa kwa ubia kati ya serikali (NARCO) na kampuni
ya National Investment Company Limited (NICOL) ambapo kwa pamoja
wameunda kampuni ya Tanzania Meat Company (TMC).
Katika
ziara hiyo Mkuu wa Mkoa alibaini sekta hiyo ya uchinjaji katika
Manispaa ya Dodoma inakabiliwa na tatizo kubwa la uchinjaji kiholela nje
ya Machinjio hiyo iliyopewa jukumu la uchinjaji mifugo (Ngombe, Mbuzi,
Kondoo) kisheria ndani ya Manispaa ya Dodoma jambo ambalo ni hatari sana
kwa usalama wa afya za walaji na kukosesha serikali mapato.
Katika
kuendesha vita hiyo ya kukomesha tabia ya uchinjaji mifugo kiholela
katika Manispaa ya Dodoma, Mhe. Gallawa amewataka wataalamu wa mifugo wa
Mkoa na Manispaa ya Dodoma kwa kushirikiana na Kampuni ya TMC kuendesha
mazoezi ya ukaguzi kwenye maeneo yote yanayohusishwa na uchinjaji
holela na kuwachukula hatua wote watakao bainika kufanya hivyo kwa kuwa
wanapingana na sheria za Afya na Mazingira.
Mhe.
Gallawa ametaka mazoezi hayo ya ukaguzi kuwa endelevu na kuhusisha hadi
ngazi za msingi za Mamlaka za Serikali za Mitaa kwenye Manispaa ya
Dodoma na kuagiza awe anapewa mrejesho kila mara ukaguzi huo
utakavyokuwa ukifanyika.
Taarifa
iliyotolewa na uongozi wa Machinjio inaeleza kuwa moja ya changamoto
kubwa zinazokabili sekta ya uchinjaji mifugo katika Manispaa ya Dodoma
ni uchinjaji kiholela nje ya Machinjio hiyo ya kisasa iliyoko Kizota
ambayo ndio imepewa jukumu kisheria la kuchinja katika Manispaa ya
Dodoma.
Taarifa
hiyo inaongeza kuwa mara nyingine mifugo hususan Ngombe wanaochinjwa
kiholela hua wagonjwa ama Ng’ombe wa wizi na hua wanachinjiwa maporini,
mafichoni, minadani ama wengine wanakwepa ushuru. Vilevile taratibu za
uchinjaji zinakuwa za kienyeji haziendani na kanuni za Afya na Mazingira
na wakati mwingi hakuna ukaguzi wa madaktari wa mifugo kuthibitisha
kama nyama zinafaa kwa matumizi ya binadamu/Kuliwa lakini cha kushangaza
nyama hizo zinauzwa maeneo mbalimbali ya mji wa Dodoma.
Taarifa
ya uongozi wa Machinjio ilimaliza kwa kusema changamoto nyingine ni
upatikanaji wa mfugo bora kwa ajili ya kuchinja machinjioni hapo kwani
kwa sasa soko na mahitaji yake ni makubwa sana kutoka nchi za kiarabu
kama Oman, Dubai, Quwait na nchi ya China na hata ndani ya nchi.
Mwanzoni
mwaka 2004 machinjio ilianza kwa kuchinja Mbuzi 200 na Ng’ombe 50 kwa
siku lakini kwa mwaka 2014 ilipanda kufikia mbuzi 1200 na Ng’ombe 150
kwa siku na malengo ya mwaka huu 2015 ni kufikia mbuzi 2000 na ngombe
300 kwa siku na kuwa ngombe wote hao ni kwa ajili ya matumizi ya ndani
pekee isipokuwa mbuzi wengi ni kwa ajili ya usafirishaji.
No comments:
Post a Comment