Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akitoa hotuba ya kufunga kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17,
2014 jijini Arusha.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akisaini Azimio la Arusha kwa niaba ya
Serikali ya Tanzania ambalo lilipitishwa wakati wa kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17,
2014 jijini Arusha.
Katibu
Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile akisoma Azimio la Arusha
linalohusu Kinga ya Jamii, alisema kuwa historia imejirudia ambapo
yapata miaka 47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la
Arusha lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi
na umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni
maadui wa taifa.
Muwakilishi
wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la shukrani wakati wa
kufunga kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii
lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha na aliisifu na kuipongeza
Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni
wanawake, wanaume na watoto pamoja na bara la Afrika na watu wake.
Naibu
Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamaii Dkt. Steven Kebwe akisistiza jambo
wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii
lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
Katibu
Mkuu Wizara ya Kazi, Mifuko ya Hifadhi ya Jamii na Huduma Ali N. Ismail
(kushoto) kutoka Kenya akifuatilia mada wakati wa kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17,
2014 jijini Arusha.
Naibu
Waziri wa Fedha Adam Malima akisistiza jambo wakati wa kongamano la
Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17,
2014 jijini Arusha.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa kwanza kulia) akifuatilia mada wakati
kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza
Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha. Kushoto ni Valentina Barca kutoka
Oxford.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum (wa kwanza kushoto) akifuatilia mada wakati
kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza
Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha. Kulia ni Waziri wa Elimu na Mfunzo ya
Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa.
Baadhi
ya wajumbe wa kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya
Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha akifuatilia mada
wakati wa kongamano hilo.
Waziri
wa Elimu na Mfunzo ya Ufundi Dkt. Shukuru Kawambwa (kushoto) akiteta
jambo na Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt. Servacius Likwelile (kulia)
mara baada ya kumalizika kongamano la Kimataifa la siku tatu kuhusu
Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
Waziri
wa Fedha Saada Mkuya Salum akiwa kwenye picha ya pamoja na baadhi ya
viongozi wa Serikali ya Tanzania na washiriki wa kongamano la Kimataifa
la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini
Arusha akionesha nakala ya Azimio la Arusha alilosaini kwa niaba ya
Serikali.
Mwakilishi
wa Umoja wa Mtaifa (UN) nchini Alvaro Rodriguez akimpongeza Waziri wa
Fedha Saada Mkuya Salum baada ya kusaini Azimio la Arusha kwa niaba ya
Serikali ya Tanzania wakati wa kongamano la Kimataifa la siku tatu
kuhusu Kinga ya Jamii lililoanza Disemba 15-17, 2014 jijini Arusha.
Na Eleuteri Mangi-Arusha
Tanzania
imepitisha Azimio linalohusu Kinga ya Jamii lenye msingi imara wa
kusimamia masuala hayo nchini na Afrika kwa ujumla ili kuwa na
maendeleo halisi kwa watu wake.
Azimio
hilo limepitishwa na kusainiwa na Waziri wa Fedha Saada Mkuya Salum kwa
niaba ya Serikali jijini Arusha wakati wa kufunga kongamano la
kimataifa la siku tatu kuhusu Kinga ya Jamii ambalo lilishirikisha
wajumbe kutoka nchi mbalimbali za Afrika na nje ya Afrika.
Akitoa
hotuba ya kufunga kongamano hilo Waziri Saada alisema kuwa maazimio
yaliyofikiwa katika kongamano hilo yametoa mwelekeo na msingi wa
kuimarisha kinga ya jamii kwa wananchi.
“Nafurahi
kusema kongamano hili limekuwa hatua muhimu katika kutekeleza masuala
ya kinga ya jamii kwa nchi zote washiriki wa kongamano hili na Afrika
kwa ujumla” alisema Waziri Saada.
Waziri
Saada alisema kuwa maazimio yaliyofikiwa wakati wa kongamano hilo
jijini Arusha yanalenga kutumia mbinu mablimbali ili kufikia malengo
yaliyokusudiwa ya kuboresha huduma za jamii kwa wananchi ikiwemo elimu
bora, afya, upatikanaji wa maji safi na salama.
Kutokana
na malengo hayo, Serikali ya Tanzania iko mstari wa mbele katika
kuwekeza na kusimamia masuala ya kinga ya jamii kwa kuwa na bajeti
endelevu ili kufikia malengo yaliyokusudiwa katika kukuza uchumi na
kupunguza umaskini kwa wanchi wake.
Akisoma
Azimio hilo la Kinga ya Jamii, Katibu Mkuu Wazara ya Fedha Dkt.
Servacius Likwelile alisema kuwa historia imejirudia ambapo yapata miaka
47 (1967-2014) iliyopita Tanzania ilipitisha Azimio la Arusha
lililolenga kupambana na maadui watatu ambao ni ujinga, maradhi na
umaskini ambao Baba wa Taifa Mwl. Julius Kmbarage Nyerere aliwaita ni
maadui wa taifa.
Maazimio
mengine yaliyofikiwa katika kongamano hilo ni kupunguza umaskini na
kukuza mitaji ya rasilimali watu ambapo Tanzania Bara inalenga ifikapo
mwaka 2025 iweimepunguza tatizo la umaskini kwa watu wake wakati
Tanzania na kwa upande wa Zanzibar inalenga kufikia hatua hiyo mwaka
2020.
Maazimio
mengine ni kuwa utawala bora ambapo Tanzania imesisitiza kuendelea
kuimarisha nguvu na sauti ya wananchi katika masuala ya kidemokrasia
nchini na kutoa na kusimamia haki za watoto, wanawake na wanaume kwa
kupinga ukatili wa kijinsia, ndoa za utotoni, mimba za utotoni pamoja na
uvamizi na mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi na mauaji ya wazee.
Kwa
upande wake Muwakilishi wa UNICEF nchini Dkt. Jama Gulaid akitoa neno la
shukrani aliisifu Tanzania kwa kuanza mapema kusimamia masuala ya kinga
ya jamii ikiwemo mifuko ya hifadhi ya jamii na misaada inayotolewa na
Mfuko wa Maendeleo ya Jamii (TASAF) kupitia mpango wake wa kunusuru kaya
maskini zilizo katika mazingira hatarishi.
Aidha,
Dkt. Gulaid aliipongeza Tanzania kwa kuwa na wimbo wa taifa
unaozungumzia watu akiwataja kuwa ni wanawake, wanaume na watoto pamoja
na bara la Afrika na watu wake licha ya kuwa na vivutio vizuri vya mlima
Kilimanjaro, hifadhi ya Serengeti na visiwa vya karafuu.
“Wimbo
huu wa Tanzania tofauti na nyimbo za nchi nyingine ambazo wao
wanazungumzia askari, watumwa, watawala wakiwemo Malkia na
Wafalme”alisema Dkt. Gulaid.
Dkt.
Gulaid aliwahakikishia wajumbe wa kongamano hilo kuwa wote wapo salama
na wapo kwenye mpango wa kinga ya jamii kwa kuwa wametambuliwa na
kubarikiwa na wimbo wa taifa wa Tanzania ambapo wajumbe waliimba wimbo
huo na kuhitimisha kongamano hilo.
Kongamano
hilo liliandaliwa na Serikali ya Tanzania kupitia Wizara ya Fedha,
Idara ya Kuondo Umaskini kwa kushirikiana na UNICEF, ILO, UNAIDS na EPRI
ambapo washiriki wa konngamano hilo wanatoka katika nchi za Kenya,
Uganda, Bangladesh, Afghanistan, Msumbiji, Lesotho, Malawi, Afika
Kusini, Ghana, Ethiopia, Zambia, Zimbabwe na mwenyeji Tanzania.
No comments:
Post a Comment