Miss
Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na Miss Kinondoni Maria Shila
wakiwa wamembeba mtoto aliekuwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima
cha New Life cha Boko, mtoto huyo alifikishwa hapo akiwa na siku nne tu
tangia kuzaliwa kwake.
Miss
Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akimkabidhi zawadi ya mwaka mpya
Msimamizi wa kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo
Boko, Mwanaisha Magambo kwa ajili ya watoto 102 waliopo kituoni hapo,
tukio hilo lilifanyika juzi.
Sehemu ya Watoto wanaolelewa katika kituo cha kulelea watoto yatima cha New Life kilichopo Boko,wakimsikiliza Miss Tanzania Lilian Kamazima.
Miss Tanzania Lilian Kamazima (kulia) akiwa na watoto katika kituo cha New Life cha Boko.
Redds
Miss Tanzania 2014 Lilian Deus Kamazima jumapili iliyopita alitoa
misaada ya vyakula vya aina mbalimbali kwa kituo cha New Life Orphans
Home kilichopo eneo la Boko nje kidogo ya jiji la D’salaam.
Kituo
hicho ambacho kilianzishwa mwaka 2005 awali kilikuwa maeneo ya magomeni
makuti kilianza na watoto yatima 17 na baadae kuongezeka hadi kufikia
70. Na kulazimika kuhama eneo hilo na kuhamia kigogo ambapo waliishi
eneo hilo hadi hivi karibuni walipopata mfadhili mmoja kutoka nchini
Qatar ambaye amewajengea jumba moja kubwa na la kisasa eneo la Boko
Dawasa, alisema bi Mwanaidi Magambo ambaye ni Mlezi wa Kituo hicho.
Kituo
hicho kina watoto wapatao 105 ambapo 60 kati yao ni wasichana na 45
wavulana. Kituo hicho kinalea watoto wadogo kabisa wa umri wa mwezi
mmoja hadi miaka 18. Hivi karibuni tulimpokea mtoto mwenye umri wa siku 5
kutoka hospitali ya wilaya ya Temeke ambaye mama yake alifariki mara tu
baada ya kujifungua, alisema bi. Magambo.
Kituo
hicho kwa sasa kina matatizo ya vyakula, vitanda, magodoro, madaftari
pamoja na sare za shule kwa ajili ya watoto hao yatima. Bi Magambo
alimshukuru sana Mfadhili huyo kutoka nchi ya Qatar kwa kuwajengea jengo
hilo, lakini alisema kwa sasa watahitaji mfadhili wa kuwalipia bili za
umeme na maji pamoja na mahitaji mengine kituoni hapo.
Kituo
hicho kina bahati ya kutembelea na warembo wa Miss Tanzania ambapo mwaka
2007, Miss Tanzania 2000 Jacqueline Ntuyabariwe alitembelea kituo
hicho wakati bado wapo eneo la Magomeni Makuti na kuwapatia misaada
mbalimbali.
Miss
Tanzania 2014 Lilian Kamazima alikabidhi vyakula vya aina mbalimbali
ikiwemo mchele, unga wa ngano, sembe, sukari, maharage, mafuta ya
kupikia, sabuni, soda, juisi, maji ya kunywa, na biskut vyote vikiwa na
thamani ya shilingi milioni mbili.
Miss
Tanzania 2014 Lilian aliishukuru kampuni ya Swissport Tanzania ambao
ndio waliofadhili ziara yake hiyo, na kuwaomba watanzania wengine
kujitokeza kwa wingi kusaidia watoto yatima na wengine wanaoishi katika
mazingira magumu.
Ziara
hiyo ya mrembo wa Taifa Lilian ilikuwa ni zawadi ya sikukuu za mwisho wa
mwaka ambao ililenga kuwafariji watoto waliopoteza wazazi wao kwa namna
moja au nyingine, na pia kutimiza Kauli mbiu ya mashindano ya urembo ya
Miss Tanzania isemayo [Beauty with Purpose] Urembo na Malengo.
No comments:
Post a Comment