Biashara na Uchumi : NBC yazindua mashine za ATM za kuweka pesa (Deposit Account) - Wazalendo 25 Blog

Habari Mpya

Glory to Story.


Post Top Ad


30 Dec 2014

Biashara na Uchumi : NBC yazindua mashine za ATM za kuweka pesa (Deposit Account)


Meneja wa ATM na Kadi wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Wambura John (kushoto) akiweka pesa kwa kutumia ATM katika hafla ya uzinduzi wa huduma ya kuweka pesa (deposit) kwa kutumia mashine za ATM ya benki ya NBC jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni mteja wa benki hiyo, Francis Xavier na kulia ni Meneja Huduma za Jamii wa NBC, Irene Peter
Mteja wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Francis Xavier (kushoto) akiweka pesa (deposit) katika mashine ya ATM ya benki hiyo wakati wa uzinduzi rasmi wa huduma hiyo jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. Katikati ni Meneja wa ATM na Kadi wa NBC, Wambura John (katikati) na Meneja Huduma za Jamii wa benki hiyo, Irene Peter.
BENKI ya Taifa ya Biashara (NBC) imezindua huduma mpya ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM jijini Dar es Salaam katika juhudi za benki hiyo kuboresha huduma za kifedha nchini.
Kuanzishwa kwa huduma hiyo kunathibitisha malengo ya benki hiyo ya kutoa huduma sahihi na ya wakati kwa wateja wake nchini nzima na huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itakuwa ikipatikana masaa 24 kila siku.
“Uanzishwaji wa huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM itawahakikishia wateja wetu kupata huduma sahihi na ya uhakika wakati wowote, uwekaji wa fedha katika mashine hizi ni wa haraka, rahisi, na inaokoa muda wa kupanga foleni ndani ya benki,” alisema Mkuu wa Njia Mbadala za Kibenki wa NBC, Raymond Mutagahywa.
Aliongeza kwamba huduma hii ya NBC kwa mtumiaji yeyote ni ya kirafiki na rahisi sana ni kwamba mtu anahitajika kufanya mambo machache tu baada ya kuingiza kadi yake ya ATM na kuchagua sehemu ya kuweka fedha na mashine ya ATM itafunguka ili mteja aweze kuweka fedha zake.
Benki hii ya NBC imeanza huduma hiyo kwenye matawi yake ya jijini Dar es Salaam, karikaoo, kinondoni, Mlimani City na Tawi la Makao makuu ambayo mteja anaweza kuweka mpaka shilingi za kitanzania 1.5milioni kwenye mashine za ATM.
Uzinduzi huu wa kuweka fedha kwenye mashine za ATM ulifanyika katika Tawi la benki hiyo la Mlimani city na kushuhudiwa na wateja kadhaa wa benki hiyo na walivutiwa na jisni mashine zinavyotumika kuweka fedha moja kwa moja.
“Hizi mashine za ATM zimekuja wakati muafaka kabisa hasa kwa wateja wetu ambao wanaendelea na biashara zao wakati ambao matawi mengi yamekuwa yamefungwa lakini huduma hii itawawezesha kufanya shughuli zao za kibenki za kuweka fedha bila matatizo,’ aliongeza Neema Munisi Mhasibu wa Tawi la Mlimani City.
“Tumeanzisha na kuzindua huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine za ATM kwenye matawi manne tu jijini Dar es Salaam na tutaendelea kufungua na kusambaza huduma hii ya kuweka fedha kwenye mashine hizi nchini nzima,” aliongeza Munisi
Kwa wake Mteja wa benki hiyo aliyejaribu huduma hiyo mpya, Franscis Xavier Momanyi alisema kwamba kwa huduma hiyo mpya kutoka benki hiyo itawahikishia wateja wote uhakika wa kupata fedha au kuweka fedha wakati wowote pindi watakapohitaji.
Alisema kwamba ni muhimu kwa benki hiyo kupeleka kwa haraka huduma hiyo ya kipekee kwenye matawi mengine nje ya mkoa wa Dar es Salaam ili wateja wengine wapate fursa ya kutumia huduma hiyo.

No comments:

Post a Comment

Post Top Ad