Kaimu
Mkurugeni wa Elimu na Huduma wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Allan
Kiulla (kulia) akizungumza machache kabla ya kumkaribisha Mgeni rasmi
kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi lililofanyika leo
kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.Bonanza hilo
lililogeshwa kufanyika michezo mbali mbali,ikiwepo mpira wa miguu,mpira
wa pete,kuvuta kamba na mingine mingi.Wa pili kulia ni Kaimu Kamishna
Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki ambaye ndie
alikuwa Mgeni Rasmi kwenye Bonanza hilo.Picha zote na Othman Michuzi.
Mgeni
rasmi kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki ya Mlipa Kodi ambaye ni Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki akitoa
nasaha zake kwa washiriki wa Bonanza hilo lililofanyika Novemba
15,2014 kwenye viwanja vya TCC Club,Chang'ombe jijini Dar es Salaam.
Sehemu
ya Wafanyakazi wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) na Wafanyakazi wa
NSSF ambao ni Waalikwa walioshiriki kwenye Bonanza la Ufunguzi wa Wiki
ya Mlipa Kodi wakifatilia kwa makini nasaha za Mgeni Rasmi,ambapo kauli
mbiu ya Mwaka huu ni "Risiti ni Haki Yako,Unaponunu Dai Risiti na
Unapouza ni Lazima Utoe Risiti".
Kaimu
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA),Tiagi Masamaki
akifatilia kwa makini michezo mbali mbali iliyokuwa ikiendelea uwanjani
hapo.
MC wa Bonanza akiendelea na Wajibu wake.
No comments:
Post a Comment