Mbunge Mgimwa akipongezwa baada ya kuchangia milioni 1.5 kwa radio Maria leo |
Mbunge wa Kalenga Bw Mgimwa akikabidhi laptop kwa mlezi wa kwaya Msindo mzee Mtandi |
Mtandi akifurahi na mbunge wake Mgimwa |
Furaha ya kukabidhiwa laptop |
Mbunge wa jimbo la kalenga Godfrey Mgimwa akivishwa kitenge cha Radio maria na mwenyekiti wa kamati ya kuchangia radio Maria Iringa Paschal Bella kushoto na katibu wake Martin Simangwa leo |
Mgimwa akipongezwa |
VYOMBO vya habari zatakiwa kuepuka
kupotosha umma juu ya mchakato mzima wa bunge la
katiba lililomalizika jana mjini Dodoma.
Kauli hiyo imetolewa leo katika viwanja
vya kanisa la Rc Mshindo na mbunge wa jimbo la kalenga
Godfrey Mgimwa wakati akichangia kiasi cha Tsh milioni
1.5 wakati wa harambee ya kuichangia radio Maria .
Alisema kuwa iwapo vyombo vya habari
zitatumika vibaya kuna uwezekano wa Taifa
kuingia katika machafuko kama zilizo nje nyingine na
kama vyombo vya habari vitafanya kazi yake kwa kuzingatia
misingi ya maadili jamii itaunganishwa na vyombo hivyo.
“ Radio Maria ni moja kati ya radio ambazo nimekuwa
nikizifuatilia toka nikiwa mdogo na nimekuwa
nikipenda zaidi jinsi radio hiyo inavyofanya
shughuli zake na mbali ya kufanya kazi ya kueneza injili
bado imekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha umma…….
Hivyo rai yangu kwa radio maria ni kuona
inaendelea hivyo hivyo na ikiwezekana kuandaa vipindi
kwa ajili ya elimu kwa umma juu ya katiba mpya “
Alisema kuwa wajumbe wa bunge la katiba wametimiza
kazi yao ambayo umma ulitegemea kutoka kwa
wajumbe hao hivyo kazi iliyobaki ni ya wananchi
kucha kuipitisha katiba hiyo mwaka 2016 na kuwa kwa
wakati huu ni vema vyombo vya habari kuendelea
kutoa elimu kwa umma juu ya kazi nzuri iliyofanywa na
bunge hilo la katiba .
Hata hivyo alisema ni vema watanzania
kuepukana na watu wachache wasiolitakia mema Taifa
ambao wanataka kuona nchi haitawaliki kwa kutaka
maandamano yasio na tija kwa jamii.
Mgimwa alisema kuwa njia pekee ya kuepukana na
viongozi wasio litakia mema taifa ni pale
ambapo vyombo vya habari vitakapoweka msimamo wa uzalendo kwa
kuepuka kuwa sehemu ya kuhamasisha kuvunjika kwa amani
nchini.
Kwa upande wake mwenyekiti wa kamati ya maandalizi ya
harambee hiyo Bw Pascal Bella akishukuru kwa mchango huo
wa mbunge Mgimwa alisema kuwa mbali ya kuwa
mbunge huyo ni wa jimbo la kalenga ila amekuwa
msaada mkubwa kwa kufanikisha zoezi hilo la kuichangia radio hiyo.
Bella alisema kuwa kila
mwaka na kila wakati wadau wa Radio maria
wamekuwa na utaratibu wa kuichangia radio hiyo
ambayo uendeshaji wake unategemea michango kutoka
kwa wadau mbali mbali na kuwa kwa mwaka huu mkoa wa
Iringa pekee unataraji kuchangia zaidi ya Tsh milioni 30
|
No comments:
Post a Comment