Afisa
Miradi ya Mawasiliano, Habari na Tehama wa shirika la kimataifa la
sayansi, elimu na utamaduni (UNESCO) Bwana Al Amin Yusuph akielezea
madhumuni ya warsha ya wadau wa mradi wa uchaguzi 2015 unaolenga
kuboresha demokrasia amani nchini katika kipindi hiki kuelekea uchaguzi
mkuu ujao, unaofadhiliwa na Shirika La Kimataifa la Maendeleo (UNDP)
ulioenda sambamba na mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya
Kijamii nchini (COMNETA).
*********************************************
Na Mwandishi wetu
Uchaguzi
huru na wa haki utafanikiwa iwapo wananchi watapewa elimu sahihi ya
uraia na upigaji kura itakayohamasisha wapiga kura kufanya maamuzi
sahihi wakati wa uchaguzi.
Hayo
yamesemwa na Kamishna wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) Jaji John
Mkwawa kwenye washa ya siku nne ya wadau wa utekelezaji wa mradi wa
uchaguzi unaolenga kuboresha demokrasia na amani nchini kuelekea
uchaguzi mkuu ujao .
Kamishina
alisema elimu ya uraia ni muhimu kwa wananchi ili kuwahamasisha
ushiriki wao katika demokrasia na kwamba haipaswi kuwa na utashi wa
kisiasa au upendeleo kwa chama chochote cha siasa.
Akitoa
mada katika warsha hiyo inayofadhiliwa na shirika la Umoja wa Mataifa
linaloshughulikia maendeleo (UNDP) Jaji Mkwawa alisema katika kutoa
elimu hiyo wanahabari hawana budi pia kuzingatia miongozo iliyowekwa ya
kutofungamana upande wowote kisiasa na kutoa habari kwa usahihi
kuhakikisha kwamba makundi yote yanapewa fursa na haki sawa.
Mwakilishi
wa Mkurugenzi Mkazi wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo (UNDP) Godfrey
Mulisa akisoma risala ya ufunguzi wa warsha hiyo kwa niaba ya Philippe
Poinsot inayoendelea kwenye ukumbi wa mikutano ofisi ya Waziri Mkuu
mjini Dodoma.
***************************************
“Pamoja
na changamoto zinazozikabili redio jamii, zina mchango mkubwa katika
mchakato wa uchaguzi kwa sababu idadi kubwa ya Watanzania hawajui kusoma
na kuandika hivyo kutegemea redio. Kwa misingi hiyo ni vyema kwa
waandishi wa habari wa redio jamii kusaini mwongozo wa maadili ambayo
yataonyesha utekelezaji wao kwa kutopendelea chama chochote cha siasa au
mgombea yoyote yule ”.
Amependekeza
pia umuhimu wa kuielewa jamii inayolengwa wakati wa kutayarisha vipindi
vya elimu ya uraia na utekelezaji ili taarifa zinazotolewa kwao
zikidhi matakwa ya sehemu hiyo.
Kamishna
wa Tume ya Taifa ya Uchaguzi Jaji John Mkwawa ametoa mfano wa kuilewa
jamii kuwa ni pamoja na kufahamu sababu zinazowafanya wananchi
wasijitokeze kwa wingi katika upigaji kura iwapo kunasababishwa na
ukosefu wa taarifa muhimu na sahihi, kukosa motisha ya kupiga kura,
utashi na kutokuwepo kwa ushindani katika kugombea.
“Katika
uchaguzi mkuu mwaka 2010 watu wachache sana walijitokeza kupiga kura
pamoja na jitihada zote za kuhamasisha na kuelimisha upigaji kura, na
baadhi ya sababu ni kwamba kupiga kura hakutampa faida yoyote mpiga
kura, au kupiga kura hakutaleta mabadiliko yoyote na kutouamini mfumo
mzima wa uchaguzi”.
Mwenyekiti
wa mtandao wa vyombo vya habari vya kijamii Tanzania (COMNETA) ambaye
pia ni Mkurugenzi wa Redio ya Jamii FADECO wilayani Karagwe, Bw.Joseph
Sekiku akieleza kwa ufupi maendeleo ya COMNETA wakati wa sherehe za
ufunguzi za mkutano wa tano wa Mtandao wa vyombo vya habari vya Kijamii
nchini (COMNETA) unaofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa ofisi ya
Waziri Mkuu mjini Dodoma.
No comments:
Post a Comment