AFYA ZETU : TUWAPELEKE WATOTO WETU KATIKA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA OKTOBA 18-24 - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Wednesday, 8 October 2014

AFYA ZETU : TUWAPELEKE WATOTO WETU KATIKA CHANJO YA SURUA NA RUBELLA OKTOBA 18-24


SURUA na rubella ni magonjwa hatari yanayoenezwa haraka kwa njia ya hewa, kutoka kwa mtu mwenye vimelea vya ugonjwa huo kwenda kwa mwingine.

Wataalamu wa afya wanaeleza kuwa dalili za magonjwa haya mawili zinafanana, hivyo ni vigumu kutofautisha. Wataalamu hao wanasema dalili kuu ni homa na vipele vidogovidogo.

Chanjo ya surua-rubella hutoa kinga kamili dhidi ya magonjwa haya. Dozi ya kwanza hutolewa kwa mtoto anapofikia umri wa miezi 9 na dozi ya pili akiwa na mwaka mmoja na nusu (miezi 18).

Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, imekutana na wadau wake wa masuala ya chanjo jijini Dar es Salaam jana, kuzungumzia mkakati wa kampeni za chanjo ulio na lengo la kuwafikia walengwa wengi zaidi ili kuongeza idadi ya watu wenye kinga dhidi ya magonjwa ya surua na rubella. 
Endelea kusoma zaidi hapa : FATHER KIDEVU BLOG

No comments:

Post a Comment