Mkuu
wa Rasilimali Watu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Flora Lupembe
(kulia) akimwagiwa maji baridi na Kaimu Mkuu wa Masoko na Mawasiliano wa
benki hiyo, Rukia Mtingwa katika hafla ya kumwagiana maji baridi
iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya kuchangisha fedha kwa
ajili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo
imefanyika jijini Dar es Salaam.
Kaimu
Mhazini Mkuu wa Benki ya Taifa ya Biashara (NBC), Ivan Tarimo (kushoto)
akimwagiwa maji baridi na mmoja wa mfanyakazi mwenzake katika hafla ya
kumwagiana maji baridi iitwayo ‘Ice Bucket Challenge’ yenye makusudi ya
kuchangisha fedha kwa ajili ya kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na
ugonjwa wa fistula. Hafla hiyo imefanyika jijini Dar es Salaam.
Mkuu
wa Kitengo cha Wateja Binafsi wa Benki ya NBC, Mussa Jallow (katikati)
naye akimwagiwa maji baridi ili kutimiza azma ya benki hiyo katika
kutafuta fedha ili kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na tatizo la ugonjwa
wa fistula nchini.
Mkuu wa Kitengo cha Mikopo Binafsi na biashara ndogondogo na za kati, Isidori Msaki (katikati) akijitahidi kujizuia wakati wafanyakazi wenzake wakimmwagia ndoo za maji baridi katika hafla hiyo.
Kaimu
ofisa mwendeshaji mkuu wa benki ya nbc, Jamie Loden akijimwagia maji
baradi ili kusaidia harakati za benki hiyo kuchangisha fedha katika
tukio hilo liitwalo ‘Ice Bucket Challenge’ kusaidia wanawake
wanaokabiliwa na ugonjwa wa fistula. Kiasi cha fedha kitakachopatika
kitapelekwa katika Hospitali ya CCBRT kwa madhumuni hayo.
Mkurugenzi
wa Fedha wa Benki ya NBC, Jaffari Matundu (kushoto) akimwagiwa maji na
mfanyakazi mwenzake katika tukio la Ice Bucket Challenge lenye lengo la
kukusanya fedha kusaidia wanawake wanaosumbulia na ugonjwa wa fistula.
Baadhi
ya wakazi wa jiji waliojitokeza kushuhudia tukio la Ice Bucket
Challenge la benki ya NBC wakiwa hawaamini macho yao wakati wafanyakazi
wa benki hiyo walipoamua kujimwagia maji baridi ili kutafuta fedha
kusaidia wanawake wanaosumbuliwa na ugonjwa wa fistula.
No comments:
Post a Comment