Rais Uhuru Kenyatta akiwa ndani ya gari la mmoja wa washiriki wa Safari Rally baada yake kuzindua mbio hizo uwanja wa KICC, Nairobi Septemba 12, 2014. Picha/PSCU
Na JABRIL ADAN na JOHN KIMWERE
Kwa Mukhtasari
Rais
Uhuru Kenyatta, ameahidi kufufua mbio za magari za kila mwaka za Safari
Rally kuhakikisha zinarejea kwenye kalenda ya mbio za kimataifa za
magari duniani. “Safari Rally imeiletea taifa hili sifa tele, kwa sasa
hakuna kupoteza muda wowote lazima kuirejeshe hadhi yake," akasema.
RAIS Uhuru Kenyatta, Ijumaa alisema
serikali itafanya juhudi kuhakikisha washiriki wa mbio za Safari Rally
wamerejea kufuzu kushiriki kampeni za mataji ya dunia. Aidha alisema
serikali yake itatoa ufadhili kwa washiriki wa mbio za Safari Rally
kuwafanya wafurahie kushiriki katika mbio hizo.
“Tunataka
kurudisha mbio hizo katika kiwango zilizokuwa hapa nyuma kiasi cha
kuwapa washiriki wazo furaha tele hasa kufuzu kushindania mataji makuu
duniani,” alisema. Rais alisema haya kwenye ukumbi wa kitaifa wa KICC
alipozindua mashindano ya KCB Safari Rally makala ya 62.
Aidha rais Kenyatta
alisema, mbio za Safari Rally zimekuwa maarufu kwa muda mrefu katika
miaka ya hapa awali kwenye kalenda ya michezo duniani. “Safari Rally
imeiletea taifa hili sifa tele, kwa sasa hakuna kupoteza muda wowote
lazima kuirejeshe hadhi yake.”
Mbio hizo
zilikuwa kwenye kalenda ya mashindano ya kimataifa hadi 2003 pale
zilizoondolewa kutokana na maandalizi mabaya na mipango duni.
Rais
alipeperusha bendera ya taifa kwa magari matatu ya kwanza na kuwatakia
washiriki heri njema kwenye kampeni za mashindano hayo. Aidha alitoa
mwito kwa Wakenya kujitokeza kwa wingi kutazama mbio za magari hayo na
kuchukua tahadhari kuzuia kutokea kwa ajali.
“Nawaomba
watazamaji kuunga mkono mchezo huu, lakini kuwa makini raha isiwazidi
kusudi kuzuia kutokea kwa ajali,” alidokeza. Rais alitoa mwito kwa
wazazi kuhakisha usalama kwa watoto wao kwenye barabara zitakazotumika
na washiriki mbio hizo.
Usalama
Mbio za
Safari Rally ni mchezo maarufu kwa muda mrefu ambapo Kenya imekuwa
ikishiriki mapambano ya viwango vya haiba kubwa duniani. Mwanzilishi wa
taifa hili, Jomo Kenyatta aliweka historia mwaka 1968 kwa kuzindua
mchezo wa kimataifa kwa mara ya kwanza.
Gavana wa
Kaunti ya Nairobi, Evans Kidero akizungumza kwenye hafla ya Ijumaa
alishauri watazamaji kufurahia mchezo huo na kuhakikisha usalama wao.
Waziri wa usalama wa Ndani, Joseph Ole Lenku aliyewakilisha Waziri wa
Michezo, Hassan Wario pia alizungumza kwenye hafla hiyo. Chanzo :Taifa Leo
No comments:
Post a Comment