Frank Mvungi- Maelezo
Serikali
yawatahadharisha wananchi kuhusu matumizi mabaya ya Mawasiliano na
udanganyifu katika usajili wa namba za simu za mkononi kwa kuwa ni kosa
la jinai.
Akizungumza
na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, Meneja Mawasiliano
wa Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) bw. Innocent Mungy amesema
kumekuwa na watu wachache wanaotumia mawasiliano pasipo kuzingatia
sheria na kanuni.
Kumekuwa
na matukio yanayoashiria kutumika kwa mitandao ya kijamii kuleta
madharambalimbali kwa watumiaji ikiwemo utapeli,kulipiza kisasi,
ugomvi,kuwaumiza wengine kwa mambo yasiyo na ukweli na kuvuruga kwa
ujumla alisema Mungy
Akifafanua
Mungy amesema pamoja na maendeleo chanya katika Sekta ya Mawasiliano
kumekuwa na watu wachache wanaotumia simu,mitandao ya
kijamii,redio,televisheni, na mawasiliano mengine kwa lengo la kuvuruga
amani.
Kutokana
na hali hiyo Mungy amesema kuwa TCRA inawakumbusha wananchi wote kwamba
ni kosa la jinai kutumia mawasilano vibaya kama ilivyoainishwa
kwenye sheria ya mawasiliano ya kielektroniki na Posta ( EPOCA) ya
mwaka 2012.
Pia
Mungy alitoa wito kwa wananchi na watumiaji wa simu za mkononi kuunga
mkono juhudi za Serikali ili wananchi wote wasajili namba za simu kwa
ajili ya kudumisha na kuendeleza amani ,usalama na kuharakisha maendeleo
ya sekta hii na Taifa kwa ujumla.
Naye
Naibu Mkurugenzi Masuala ya Huduma kwa wateja toka mamlaka hiyo Bw.
Isaac Mruma amesema ni vyema wananchi wakazingatia matumizi sahihi ya
mawasiliano kwa maslahi mapana na Taifa.
Sheria
ya Mawasiliano ya Kielektroniki na Posta (EPOCA) mwaka 2010, kifungu
cha 131 imeainisha kuwa ni kosa la jinai kutumia au kuwezesha kutumika
kwa namba ya simu isiyosajiliwa na adhabu yake ni faini ya shilingi laki
tano (Tsh. 500,000) au kifungo cha miezi mitatu kwa atakayekiuka sheria
hii
No comments:
Post a Comment