UFUNDI KWANZA :VETA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO MKOANI LINDI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 5 August 2014

UFUNDI KWANZA :VETA KATIKA MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE VIWANJA VYA NGONGO MKOANI LINDI


Wafanyakazi na wanafunzi wa Mamlaka ya Mafunzo ya Ufundi Stadi VETA kutoka vyuo mbalimbali nchini wapo katika maonesho ya wakulima nane nane yanayofanyika Kitaifa Mkoani Lindi katika viwanja vya maonesho Ngongo kilometya 17 kutoka Lindi mjini. VETA wamesheni vitu mbalimbali na mafunzo kwa wakulima na teknolojia za kisasa. Pia kuna mgahawa wa kisasa upo kibandani kwao na unatoa huduma zote za hoteli kuanzaia chakula na vinywaji vyote. 
 Mwanafunzi wa Uashi wa VETA, Noel Sowan akiwaonesha vijana wenzake wa Lindi namna ya ufyatuaji wa matofari ya kissa yatuamiayo udongo yanavyo fanyika.
 Huyu akijenga kwa matofali hayo na nyumba hupendeza
 Beatrice Kirati ambaye ni Mwanafunzi wa VETA akifafanua juu ya kifaa cha kisasa cha kunyeshea kuku na nyuki maji. Kifaa hicho kinaweza unganishwa na bomba au tanki la maji moja kwa moja bila kumfanya mfugaji kuwekea mifugo yake maji mara kwa mara.
 Mwanafunzi wa VETA, Jackson Range akimpa maelezo juu ya mashine ya kutotolea vifaranga iliyotengenezwa nao.
 Mtaalam wa kutathmini mafunzo ya VETA, Joyce Mwinuka akiwasikiliza maofisa wa Polisi kutoka Mkoani Lindi ambao ni Mkuu wa Kituo cha Polisi Mingoyo, Mkaguzi wa Polisi Juma Solomon (kushoto) na Mkuu wa Oparesheni wa Mkoa wa Lindi, ASP. Charles Onyango walipotembelea banda la Veta.
 Raia wa Uingereza anaefanya utalii kwa kusafiri na pikipiki kutoka nchini kwake hadi Afrika Kusini akianglia mashine ya asili ya kukeleza mbao iliyobuniwa na VETA Mtwara. Wanaompa maelezo ni Mwalimu, Juma Malibidu (kulia) na Aboubakar Maurusi.
 Raia wa Uingereza anaefanya utalii kwa kusafiri na pikipiki kutoka nchini kwake hadi Afrika Kusini akianglia mashine ya kufyatulia nishati mbada ya kupikia itokanayo na maranda ya mbao. Hii ni VETA Pekee
VETA pia ina mashine maalum za kisasa za umwagiliaji maji katika bustani yako. Picha na Mroki Mroki

No comments:

Post a Comment