Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh. Ridhiwani Kikwete akikata utepe kuzindua
maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze mjini Chalinze jana ambayo
imejengwa na Kampuni ya Tanga Cement kupitia bidhaa yake ya Simba Cement
kwa kushirikiana na taasisi ya Read International kwa gharama ya
shilingi milioni 42 za kitanzania katika kuboresha elimu jimboni humo,
Mbunge huyo pia ameahidi kujenga jiko katika shule hiyo na kuongeza
kompyuta ili wanafunzi wajengewe mzingira mazuri zaidi ya kujisomea
lakini pia ameahidi kushughulikia tatizo la wanafunzi 10 ambao wamefauru
kwenda kidato cha ano na sita lakini hawakupata nafasi ya kuchaguliwa,
hivyo ameueleza uongozi wa shule hiyo pamoja na wazazi kwamba wanafunzi
hao lazima watafutiwe nafasi ya kuendelea na shule hata kama itakuwa
siyo ndani ya jimbo la Chalinze, "Muhimu wapate nafasi ya kuendelea na
elimu yao ya kidato cha tano na sita" Alisema Mh. Ridhiwani Kikwete
alimuomba mwenyekiti wa bodi ya shule hiyo Bw. Mbwana Madeni amkabidhi
majina ya wanafunzi wote kumi ili yaanze kufanyiwa kazi mara moja.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakipata maelezo kutoka kwa
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni
kabla ya kuzindua rasmi maktaba ya shule hiyo, Katikati ni Emma Lyu
kutoka taasisi ya Read International na kushoto ni Raquel Araya kutoka
Taasisi ya Read International pia.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akionyeshwa vitabu mbalimbali
vilivyopo katika maktaba ya shule ya sekondari ya Chalinze na Najma
Juma kutoka Chuo Kikuuu cha Dar es salaam UDSM ambaye anafanya kazi za
kujitolea katika taasisi ya Read Internional.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiangalia kitabu wakati
akikagua maktaba hiyo kulia kwake ni Najma Juma wa Read International.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikweteakiweka alama za kiganja chake
kama kumbukumbu wakati alipozindua maktaba hiyo jana kwenye shule ya
sekondari ya Chalinze.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwete akifurahia jambo wakati
Mwenyekiti wa bodi ya shule ya sekondari Chalinze Bw. Mbwana Madeni
alipokuwa akisoma risala yake mbele ya mbunge huyo, kutoka kulia ni
Raquel Araya kutoa taasisi ya Read International na mkuu wa ituo cha
polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
Mbunge
wa jimbo la Chalinze Mh Ridhiwani Kikwetea akizungumza na wanafunzi wa
sule ya sekondari ya Chalinze pamoja na walimu mara baada ya kuzindua
maktaba katika shule hiyo jana kushoto ni Mbwana Madeni mwenyekiti wa
bodi ya shule, na kutoka kulia ni Raquel Araya kutoka Read International
na mkuu wa ituo cha polisi cha Chalinze Afande J.S Magomi.
No comments:
Post a Comment