Mwandishi wa habari wa Marekani aliyekatwa kichwa, James Wright Foley (kushoto), akiwa amevishwa kanzu maalum.
Kabla
ya kuuawa kwake, Foley, aliwataka marafiki, wanafamilia wake na wapenzi
wake wote kupambana na “wauaji wangu wa kweli” ambao ni serikali ya
Marekani.
Foley akiwa na muuaji wake ambaye alisema kitendo cha kumwadhibu
mwandishi huyo ni kulipiza kisasi mashambulizi ya ndege za Marekani
nchini Iraq.
Muuaji wa Foley akijitayarisha kumkata kichwa.
Foley enzi za uhai wake hadi alipopotea Novemba 2012, baada ya kutekwa huko Taftanaz, kaskazini mwa Syria.
Mama yake Foley, Diana, na baba yake John, wakiwa katika mkesha
kanisani kuwataka wapiganaji wa ISIS kuwaachia mateka wao.Kikosi cha
kiislam cha kijeshi chenye msimamo mkali kimeachilia video inayoonesha
mauaji ya mwandishi habari mwenye asili ya Marekani. James Foley
alipotea tangu
alipokamatwa mateka na kushikiliwa nchini Syria miaka miwili iliyopita na sasa ameuawa.
Ikulu ya Marekani imesema inaifanyia uchunguzi wa kina video hiyo na ikithibitika kwamba mwandishi huyo wa habari ni wa taifa hilo ,serikali ya Marekani itataka ufafanuzi wa kina ilikuaje na kwanini James Foley auawe.Picha na habari kwa hisani ya GPL
No comments:
Post a Comment