Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la Nyumba
la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo
zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. (Picha zote kwa hisani ya Kitengo cha
Mawasiliano na Huduma kwa Jamii cha Shirika la Nyumba la Taifa)
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akisalimiana na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Abdulkarim Shah.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na wafanyakazi wa Shirika la
Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo
zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akikaribishwa katika mradi wa nyumba za
gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Ardhi
Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene katika
mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani
Dodoma
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akishuhudia jiwe la msingi mara baada ya kuzindua
mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa
mkoani Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC
Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu Waziri wa
Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu,
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai,
Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika Mashariki
Adam Kimbisa.
Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu akizungumza katika hafla hiyo jana
Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Job Ndugai akizungumza katika hafla hiyo jana
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akijadiliana jambo na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika
la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu wakati akitembelea mradi wa
nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma.
Mradi huo una jumla ya nyumba 44..
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizungumza wakati akitembelea mradi wa
nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma.
Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala
Simbachawene akizungumza wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama
nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una
jumla ya nyumba 44.
Wageni waliokuwapo katika hafla hiyo
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akitoka ndani ya nyumba ya mfano baada ya
kuzindua nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa
mkoani Dodoma akiwa pamoja na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la
Taifa, Nehemia Kyando Mchechu, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli
na Mbunge wa Afrika Mashariki Adam Kimbisa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akizindua mradi wa nyumba za gharama nafuu
za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani Dodoma akiwa pamoja na Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala
Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia
Kyando Mchechu, Naibu Spika wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania,
Job Ndugai, Waziri wa Ujenzi Dk John Pombe Magufuli na Mbunge wa Afrika
Mashariki Adam Kimbisa.
Rais Jakaya Mrisho Kikwete akifunua kitambaa kuashiria uzinduzi mradi
wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo zilizopo Kongwa mkoani
Dodoma wanaoshuhudia ni pamoja na Naibu Waziri wa Ardhi Nyumba na
Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala Simbachawene na Mkurugenzi Mkuu
wa Shirika la Nyumba la Taifa, Nehemia Kyando Mchechu.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete akisalimiana na Meneja wa NHC mkoa wa Dodoma
Itandula Gambalagi wakati wa uzinduzi wa nyumba hizo za gharama nafuu.
Naibu
Waziri wa Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi, George Tuguluvala
Simbachawene akizungumza na Meneja wa NHC Dodoma Itandula Gambalagi
wakati akitembelea mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo
zilizopo Kongwa mkoani Dodoma. Mradi huo una jumla ya nyumba 44.
Rais
Jakaya Mrisho Kikwete katika picha ya pamoja na viongozi wa Shirika la
Nyumba la Taifa katika mradi wa nyumba za gharama nafuu za NHC Mnyakongo
zilizopo Kongwa mkoani Dodoma, wakati wa uzinduzi wa mradi huo
uliofanyika jjana.
Msafara wa Rais Jakaya Mrisho Kikwete ukiwasilia katika eneo la tukio
- Na Sifa Lubasi, Kongwa
- HALMASHAURI nchini zimetakiwa kununua nyumba za bei nafuu zinazojengwa na Shirika la Nyumba (NHC) ili kuwapangisha watumishi wake.
Kauli
hiyo ilitolewa jana na Rais Jakaya Kikwete alipokuwa akizindua mradi wa
nyumba nafuu katika eneo la Mnyakongo wilayani Kongwa mkoani Dodoma.
Alisema
kumekuwa na tabia ya baadhi ya maeneo watumishi wa halmashauri kukaa
mbali na sehemu zao za kazi kwa visingizio vya kukosa makazi.
Alisema
sababu hiyo sasa haina msingi katika maeneo ambayo NHC imejenga nyumba
zao kwani halmashauri inaweza kununua nyumba hizo na kuwapangisha
watumishi wake.
‘’
Hawa NHC wana utaratibu kwa kupitia mabenki wanayoshirikana nayo hivyo
kwa kutumia utaratibu huo halmashuri mnaweza kwenda katika hizo benki na
kuingia mkataba na kukopa nyumba hizo na kisa kuwapangisha watumishi…’’
alisema.
Aidha
Rais Kikwete alisema shirika hilo linafanya kazi nzuri katika ujenzi wa
nyumba hizo za bei nafuu huku akilitaka kuongeza zaidi idadi ya nyumba.
Alisema ni vyema sasa halmashuri zikaongeza maeneo ya kujenga nyumba
hizo ili wananchi wengi zaidi waweze kuishi katika nyumba bora.
Akizungumza
katika uzinduzi huo Mkurugenzi Mtendaji wa NHC Nehemia Mchechu alisema
mradi huo ni utekelezaji wa mpango wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu.
Alisema mradi huo wenye nyumba 44 hadi kukamilika utakuwa umegharimu
Shilingi bilioni 1.2.
Alisema nyumba hizo zinauzwa kwa gharama kati ya Sh milioni 35 hadi 40 kulingana na ukubwa wa nyumba husika.
Hata hivyo alisema bado kuna tatizo la kodi katika uuzaji wa nyumba hizo na ndio kinachofanya kuuzwa kwa bei kubwa.
Alimuomba
Rais kusaidia katika kusukuma nia ya kushusha kodi ili nyumba hizo
ziuzwe kwa bei nafuu na kila mwananchi aweze kununua.
No comments:
Post a Comment