Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta akizungumza na baadhi viongozi
na wajumbe kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba
Tanzania(TACOGA) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo
wakati walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Kaimu Mwenyekiti wa kutoka Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA), Godfrey Mokiri(katikati) akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta(kulia) katika ukumbi wa mikutano wa Bunge wa Pius Msekwa leo wakati baadhi viongozi na wajumbe wa chama hicho walipomtembelea ofisini kwake mjini Dodoma kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.Kushoto ni Katibu wa chama hicho, George Mpanduji.
Baadhi viongozi
na wajumbe wa Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba
Tanzania(TACOGA) wakiwa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa Bunge
Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta (wanne kushoto) na Katibu wa Bunge
hilo, Yahaya Khamis Hamad (wa tatu kulia )walipomtembelea
ofisini kwake mjini Dodoma , kwa lengo la kuwasilisha Azimio la wito
wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa rasimu
yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania. Picha na
Kamati ya Bunge Maalum la Katiba
********************************
Na Magreth Kinabo, DODOMA
Chama cha Wakulima Wadodowadogo wa zao la Pamba Tanzania(TACOGA) kimemwomba Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe . Dkt . Jakaya
Mrisho Kikwete asisitishe mchakato wa mijadala ya Bunge Maalum la
Katiba , kwani kitendo cha kusitisha ni kuzuia makusanyo ya
mawazo mtambuka ya wabunge .
Kauli
hiyo imetolewa leo na Katibu chama hicho, George Mpanduji wakati
akizungumza na Mwenyekiti wa Bunge Maalum la Katiba, Mhe. Samuel Sitta
Maalum ofisini kwake mjini Dodoma leo kwa lengo la kuwasilisha Azimio
la wito wa kuomba Bunge Maalum la Katiba kukamilisha jukumu la kuandaa
rasimu yenye kuzingatia haki ardhi kwa mahitaji ya wakulima Tanzania.
Mpanduji aliambatana
na baadhi wa viongozi na wajumbe kutoka mikoa 11 wa TACOGA
,alisema wanaheshimu makubaliano ya kisiasa ya kutungwa Katiba ya
Nchi, lakini tunatahadharisha kuwa shurti za kisiasa zinazopiganiwa na
vyama vya upinzani Bungeni hadi kuzuia wabunge kutetea haki mtambuka za
kijamii suala hilo linaleta hitilafu ya kuchelewesha mahitaji muhimu
kama ya kujengwa amani kati ya wakulima na wafugaji.
“
Vikao vya Bunge Maalum viendelee na wabunge wote watangulize kwanza
maslahi ya umma dhidi ya misukumo batili iliyo kinyume na maslahi
mapana ya umma na taifa. Wabunge hawa wanafikra chanya za kujenga
makutano ya fikra patanifu ya kupatikana suluhu za haki za makundi
mbalimbali, hususani pale palipo na ombwe la matakwa hayo Katika ya
sasa,” alisema Mokiri.
Aidha
Mpanduji aliongeza kwamba wanashauri agenda za haki mbalimbali kwa
jamii zipewe vipaumbele kwa kuwa pana vilio vya kuhitajika suluhu za
haraka kwa mahitaji mbalimbali ya makundi ya umma.
Mpanduji alisema
wakulima hao, wanataka Katiba ipatiokane haraka kwani itakuwa suluhisho
dhidi ya mizozo na maafa yanayotokea nchni kati ya wakulima na
wafugaji.
“
Tunahimiza vyama vya siasa vishindanishe hoja za kukonga mioyo kwa
kutetea haki za jamii na taifa dhidi ya kutambulisha misukumo y shurti
za utashi wa makundi ya watu ya maslahi binafsi,” alisisitiza.
Alisema
chama hicho ,pia kinampongeza Mhe. Sitta kwa uvumilivu wake na hekima
ya uongozi na wabunge wote wanaohudhuria vikao vya Bunge hilo kwa kuwa
wanatimiza uzalendo wao, uaminifu wao na utiifu wao wa kutumikia jamii
na taifa.
Chama
hicho kimtaka mlezi wao ambaye ni John Shibuda Mbunge wa Jimbo la Maswa
Maghribi, ambaye waliochagua kuanzia mwaka 2012 kuendelea kuhudhuria
vikao vyote vya Bunge hilo ili akasimamie maslahi yao na aungane na
vikundi vinavyoandaa na kutetea haki za wakulima Tanzania.
Kwa upande wake Mhe. Sitta alisema lengo la kutungahiyo ni iwe rafiki yenye kukidhi matakwa ya wananchi.
Miongoni
mwa hoja nyingine walizozungumzia ili Katiba itamke ni haki ya mikopo
kwa wakulima, ruzuku wa wakulima, iwalinde na itamke haki za wanawake
katika kumiliki ardhi wanapofiwa na waume zao na kufadika na mapato ya
kilimo.
No comments:
Post a Comment