Kamishna
Jenerali wa Jeshi Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso
Rodrudges(kulia) kabla ya kusaini Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la
Magereza na Kmapuni hiyo ya uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la
Gereza Wazo Hill leo Agosti 21, 2014 Jijini Dar es Salaam.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza John Casmir Minja(kushoto) akiwa na
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso
Rodrudges(kulia) wakisaini nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia katika
mradi wa uchimbaji madini ya chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill.
Kamishna
Jenerali wa Jeshi la Magereza, John Casmir Minja(kushoto) na Mkurugenzi
Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw. Alfonso Rodrudges(kulia)
wakibadilishana nyaraka muhimu za Makubaliano ya ubia kati ya Shirika la
Magereza na Kampuni ya Twiga Cement katika mradi wa uchimbaji madini ya
chokaa katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Baadhi
ya Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza wakishuhudia utiaji sahini
wa Makubaliano ya ubia wa mradi wa uchimbaji madini ya Ujenzi katika
Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam.
Maafisa
Wandamizi wa Jeshi la Magereza walioshiriki hafla ya utilianaji sahini
Makubaliano ya ubia huo wakimsikiliza Mtaalam Mshauri wa Kampuni ya
Twiga Cement, Bw. Said Abdallah(hayupo pichani) namna Jeshi la Magereza
litakavyonufaika na mradi huo wa madini.(Picha zote na Lucas Mboje wa
Jeshi la Magereza).
Na; Lucas Mboje
Jeshi
la Magereza nchini kupitia Shirika lake la Magereza limeingia
makubaliano rasmi ya mradi wa uchimbaji madini ya Chokaa na Kampuni ya
Saruji ya Twiga katika eneo la Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salam.
Makubaliano
hayo yamefanyika leo Alhamisi 21 Agosti, 2014 katika Ukumbi wa Mkutano
wa Makao Makuu ya Jeshi la Magereza Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza
na Maafisa Waandamizi wa Jeshi la Magereza pamoja na Wanahabari,
Kamishna Jenerali wa Magereza nchini, John Casmir Minja amesema kuwa
ushirikiano huo kati ya Shirika la Magereza na Twiga Cement unalenga
kuimarisha Shirika la Magereza ili liweze kujiendesha kibiashara kwa
kuchangamkia fursa mbalimbali za kiuchumi.
Ametaja
madini na maeneo ambayo Jeshi hilo litafanya uchimbaji madini kwa ubia
ni pamoja na Chokaa, mawe, kokoto, mchanga, zahabu na moramu katika
maeneo ya Magereza mbalimbali hapa nchini ambayo ni Maweni(Tanga),
Lilungu(Mtwara), Bahi(Dodoma), Msalato(Dodoma), Majimaji(Songea),
Kalilankulukulu(Mpanda).
“Tayari
Jeshi la Magereza limepata leseni 164 za Uchimbaji wa madini ya Ujenzi,
vito na zahabu katika maeneo mbalimbali ya magereza hapa nchini”
Alisema Kamanda Minja.
Kamishna
Jenerali Minja ameongeza kuwa upatikanaji wa leseni hizo ni mojawapo ya
hatua ya kukabiliana na changamoto mbalimbali zinazolikabili Jeshi la
Magereza, hususani katika kuipunguzia Serikali gharama za kuhudumia
magereza na kuongeza pato la Kodi kwa Taifa.
“Vyanzo
vilivyobuniwa kuongeza tija ni pamoja na kuingia ubia na Wawekezaji
wenye nia ya dhati ya kushirikiana na Jeshi letu katika madini hayo”
Alisisitiza Kamanda Minja.
Kwa
upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya Twiga Cement, Bw.Alfonso
Rodrudges amesema kuwa Kampuni yake ipo tayari kwa dhati kushrikiana na
Shirika la Magereza katika mradi huo wa uchimbaji madini ya ujenzi na
kuwa yapo mahitaji makubwa ya bidhaa hiyo katika Ujenzi wa Barabara
katika Jiji la Dar es Salaam.
“Makubaliano
haya ya ubia yataongezea uhakika wa upatikanaji wa madini ya chokaa
katika maeneo ya karibu na Kiwanda chetu hivyo kuongeza uzalishaji wa
saruji nchini na kuwa na muda mrefu zaidi(lifespan) wa kuendesha
shughuli za Kiwanda chetu” Alisema Bw. Rodrudges.
Pia
ameongeza kuwa mbali na kuliongezea mapato Jeshi la Magereza katika
mradi huo pia Kampuni yake itatoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za
kuishi Maofisa na Askari wa Gereza Wazo Hill Jijini Dar es Salaam hivyo
kupunguza changamoto kubwa ya uhaba wa nyumba za kuishi askari.
Mkakati
wa Jeshi la Magereza hivi sasa ni kuendelea kuboresha maeneo mbalimbali
pamoja na kuchangamkia fursa zilizopo ili kuhakikisha kuwa linafikia
ufanisi unaotarajiwa katika utekelezaji wa majukumu yake.
Makubaliano
hayo yatakuwa na manufaa makubwa kwa Shirika la Magereza katika kukuza
mtaji na kubadilishana ujuzi katika miradi mbalimbali ya madini hayo.
No comments:
Post a Comment