JESHI LETU : AMIRI JESHI MKUU , RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 179 WA JESHI MONDULI, ARUSHA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Monday, 25 August 2014

JESHI LETU : AMIRI JESHI MKUU , RAIS DKT. JAKAYA KIKWETE ATUNUKU KAMISHENI KWA MAAFISA WAPYA 179 WA JESHI MONDULI, ARUSHA


Amiri Jeshi Mkuu,Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpa zawadi na kumpongeza luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe baada ya kuibuka mwanafunzi bora wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni maafisa wapya 179 wa jeshi la Wananchi waliohitimu vyema mafunzo yao katika chuo cha Jeshi Monduli Mkoani Arusha jumamosi.
Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akitunuku kamisheni kwa maafisa wapya 179 wa jeshi waliohitimu vyema mafunzo yao ya muda mrefu katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha.
Maofisa wapya wa Jeshi wakila kiapo mbele ya Amiri jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete wakati wa hafla ya kuwatunuku kamisheni iliyofanyika katika chuo cha jeshi kilichopo Monduli Mkoani Arusha .
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na maofisa wapya wa jeshi baada ya kuwatunuku kamisheni katika sherehe zilizofanyika katika chuo cha jeshi Monduli mkoani Arusha.
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akimpongeza Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe aliyeibuka mwanafunzi bora(Best Officer Cadet Traineer Overall) wakati wa mafunzo ya muda mrefu ambapo maafisa 179 wa jeshi walihitimu vyema na kutunukiwa kamisheni katika chuocha jeshi Monduli .
Amiri Jeshi Mkuu Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete akiwa katika picha ya pamoja na mwanafunzi Bora katika kozi ya muda mrefu ya jeshi Luteni Usu Mohamed Ramadhani Mgalawe(watatu kushoto) pamoja na wazazi wake muda mfupi baada ya Rais Kuwatunuku kamisheni maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha Monduli Mkoani Arusha .
Mtoto mdogo akimsalimia Rais Dkt.Jakaya Mrisho Kikwete muda mfupi baada ya kumalizika kwa sherehe za kuwatunuku kamisheni Maofisa 179 wa jeshi katika chuo cha jeshi Monduli Mkoani Arusha. (picha na Freddy Maro)

No comments:

Post a Comment