Makamu
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA),Alhaji Said El-Maamry (kushoto) akiuliza jambo
kwa Meneja Miradi wa DAWASA,Ing. Romanus Mwang'ngo (kulia) juu ya Mtambo
wa Ruvu chini,wakati wa ziara yao iliyofanyika leo Agosti 20,2014.Wa
pili kulia ni Mwenyekiti wa Bodi hiyo,Dkt. Eve-Hawa Sinare
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare (wa pili kushoto) akijadiliana
jambo na Makamu wake,Alhaji Said El-Maamry (kulia) mara baada ya
kumaliza ziara ya kutembelea miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini leo Agosti
20,2014.Wengine pichani ni Wajumbe wa Bodi hiyo,Bw. Daniel Machemba
(kushoto) na Ing. Mary Mbowe (wa pili kulia)
Wajumbe
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA) wakiwa kwenye picha ya pamoja mara baada ya kumaliza
ziara yao katika Miradi ya Ruvu Juu na Ruvu chini.
Mtendaji
Mkuu wa Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam (DAWASA),Ing.
Archerd Mutalemwa akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya namna
Shirika lake lilivyojipanga kuwaondolea kabisha hadha ya maji Wakazi wa
Jijini la Dar es Salaam wakati akielezea kukamilika kwa Mtambo wa Maji
wa Ruvu chini wenye Uwezo wa kutoa maji Lita Milioni 270 kwa siku
ukitofautisha na uwezo wa Mtambo wa zamani uliokuwa ukitoa lita chache.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es
Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare akizungumza na waandishi wa habari
juu ya ziara yake hiyo aliyoambatana na Wajumbe wake wote.
Mhandishi
Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura (mwenye kizibao cha rangi ya
chungwa) akitoa maelezo ya Maendeleo ya Mradi wa Ruvu chini kwa Ujumbe
wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka Dar es Salaam
(DAWASA) uliotembelea Mradi huo Agosti 2014.
Sehemu ya Mabomba ya kusafirishia Maji katika Mtambo wa Ruvu chini.
Mhandishi Mshauri wa Kampuni ya UWP,Chacha Wambura akifafanua jambo kwa
Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugeni ya Mamlaka ya Maji Safi na Maji Taka
Dar es Salaam (DAWASA),Dkt. Eve-Hawa Sinare wakati wakitembelea sehemu
ya Mtambo wa Maji wa Ruvu chini uliomalizika matengenezo yake.
Sehemu ya visima vya Maji Ruvu chini.
No comments:
Post a Comment