Watumishi
wa TMAA wakiwa tayari kuwaelimisha na kuwahudumia wananchi waliotembelea Banda
lao kwenye viwanja vya Saba Saba.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu
uliokuwa ukioneshwa banda hapo.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu
uliokuwa ukioneshwa banda hapo.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu
uliokuwa ukioneshwa banda hapo.
Baadhi
ya wananchi waliotembelea Banda la TMAA wakishuhudia mchanga wa dhahabu
uliokuwa ukioneshwa banda hapo.
Na
Saidi Mkabakuli
Mamia
ya wakazi ya jiji la Dar es Salaam na vitongoji vya wamejitokeza kujionea
mchanga wa dhahabu unaoneshwa kwenye Banda la Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania
(TMAA) lililopo katika viwanja vya Maonesho ya Kimataifa vya Mwalimu Julius
Nyerere, jijini Dar es Salaam.
Mmoja
wa wakazi hao Bw. Shabaan Charahani, amesema ameshawishika kuja kujionea mchanga
huo na kupata ukweli juu ya kutoroshwa kwa mchanga huo kama inavyovumishwa na
watu wengi nchini.
“Nimekuja
kujifunza masuala ya ukaguzi wa madini na kujua ukweli juu ya mchanga wa
dhahabu unaozalishwa hapa nchini,” alisema Bw. Charahani.
Akitoa
maelezo kwa wananchi hao waliojitokeza bandani hapo, Afisa Habari wa Wakala
huo, Mhandisi Yisambi Shiwa alisema kuwa mchanga wa dhahabu ni zao lenye madini
ya shaba na fedha lipatikanalo mara baada ya kuchenjua mawe yenye dhahabu
kwenye mtambo wa kuchenjulia mawe hayo uliopo kwenye migodi ya Bulyanhulu na
Buzwagi.
Aliongeza
kuwa kuna mkanganyiko wa matumizi sahihi ya neno mchanga wa dhahabu, ambapo
kiusahihi mchanga wa dhahabu ni makinikia ya shaba (copper concentrate).
“Kutokana
na madini ya shaba kuwa mengi kwenye huu ‘mchanga wa dhahabu’ kuliko madini
mengine, jina rasmi linalotumika na kutambulisha zao hili ni makinikia ya
shaba,” alifafanua.
Kwa
mujibu wa Mhandisi Shiwa, kwa sasa, uzalishaji wa makinikia ya shaba unafanyika
katika migodi ya Bulyanhulu na Buzwagi tu. Akiitaja sababu ya kuwepo na aina ya
mashapo ya dhahabu ya migodi hiyo kuwa na sifa tofauti na migodi mingine
mikubwa ya dhahabu hapa nchini.
Akitaja
sababu za kusafirishwa nje ya nchi mchanga huo, Mhandisi Shiwa kwamba
kutokuwepo kwa teknolojia ya kutenganisha madini hayo, pamoja na gharama kubwa
za kuendeshea mtambo wa kufanya kazi hiyo.
“Gharama
za mtambo wa kuchenjulia madini hayo ni wastani wa dola za kimarekani milioni
500. Gharama hizi ni kubwa ukilinganisha na hali halisi ya mapato ya migodi ya
Bulyanhulu na Buzwagi yatokanayo na ‘mchanga wa dhahabu’,” alisema Mhandisi Shiwa.
Mhandisi
Shiwa aliongeza, “kutokuwepo na umeme wa uhakika na uzalishaji duni wa
makinikia hayo ndo sababu kuu za kutofanyika kwa kazi hiyo hapa nchini,”
aliongeza.
Kwa
mujibu wa takwimu zilizopo kiasi cha makinikia kinachozalishwa hapa nchini ni
wastani wa tani 45,000 ilhal kiasi kinachotakiwa ni wastani wa tani 150,000 za
makinikia ya shaba.
TMAA
ni Wakala wa Serikali ulioanzishwa tarehe 2 Novemba, 2009 chini ya Sheria ya
Wakala wa Serikali, Sura ya 245. Tamko la Waziri la kuanzisha Wakala
lilichapishwa kwenye Gazeti la Serikali Namba 362 la tarehe 6 Novemba, 2009.
Lengo la Wakala ni kuhakikisha kwamba, Serikali inapata mapato stahiki kutoka
kwenye shughuli za uzalishaji na biashara ya madini nchini kupitia usimamizi na
ukaguzi makini wa shughuli za uchimbaji, na kuhakikisha kuwa shughuli hizo
zinafanyika kwa kuzingatia uhifadhi na utunzaji thabiti wa mazingira katika
maeneo ya migodi.
No comments:
Post a Comment