Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiagana na Rais wa Malawi, Profesa Arthur Peter Mutharika, baada ya
shughuli za maadhimisho ya Sherehe ya miaka 50 ya uhuru wa Malawi
kukamilika katika uwanja wa Civo, jana Julai 06, 2014. Nyuma yake ni
Mama Asha Bilal.
Wa pili (kushoto) ni Rais wa Zimbabwe, Robert Mugabe, Rais wa Malawi Profesa
Arthur Mutharika akifuatiwa na mkewe, Mheshimiwa Makamu wa Rais wa
Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, Mama Asha
Bilal na viongozi wengine wakifuatilia sala maalum ya kuombea nchi ya
Malawi wakati wa sherehe za miaka 50 ya uhuru wa nchi hiyo zilizofanyika
jana Jumapili Julai 06, 2014 katika uwanja wa Civo jijini Lilongwe,
Malawi.
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal
akiongozana na Mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi Saulos Klaus
Chilima kukagua gwaride maalum la makaribisho kwa Mheshimiwa Makamu wa
Rais wa Tanzania baada ya kuwasili kwenye uwanja wa Ndege wa Lilongwe
kwa ajili ya kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi
zilizofanyika jana Jumapili.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na mwenyeji wake Makamu wa Rais wa Malawi, Saulos Klaus Chilima, wakifurahia ngoma za asili za
Malawi, wakati wa mapokezi kwenye Uwanja wa Lilongwe, alipowasili
kuhudhuria sherehe za miaka 50 ya uhuru wa Malawi zilizofanyika
Jumapili.
Rais wa Malawi, Profesa. Arthur Peter Mutharika, akikagua gwaride wakati wa sherehe hizo.
Askari wa Jeshi akisimamia na kuwapanga wananchi wasiingie uwanjani....
Makundi mbalimbali pia yalijitokeza kuandaa sare na kuhudhuria sherehe hizo....
Baadhi ya kinamama wakiwa katika sare ya Kitenge cha Mutarika...
Vikosi vya usalama, vikipita mbele ya Jukwaa Kuu kwa mwendo wa pole na haraka.....
Mwendo wa pole.....
Mwendo wa pole.......
No comments:
Post a Comment