NA MWANDISHI WETU, BUSEGA
MWENYEKITI
wa CCM mkoani Simiyu, Dk. Titus Kamani, amewataka viongozi wa ngazi
mbalimbali wakiwemo Madiwani, Makatibu wa Chama na Jumuia zake,
kujiwekea ratiba ya kutembelea wananchi ili watambue kero
zinazowakabili.
Dk.
Kamani, ambaye pia ni Mbunge wa Busega na Waziri wa Maendeleo ya Mifugo
na Uvuvi, alisema hayo mwishoni mwa wiki wakati akizungumza na baadhi
ya viongozi wa Chama katika Kijiji cha Lamadi wilayani Busega.
Alisema
huu sio wakati wa kukaa na kubweteka ofisini kusubiri wananchi
wapelekea kero, bali ni wakati wa kuwatembelea na kufanya mikutano na
kuwajulisha utekelezaji wa masuala mbalimbali ya maendeleo ambayo
yanatekelezwa kutokana na Ilani ya CCM.
“Madiwani
wenzangu, wenyeviti, makatibu wa Chama na jumuia zetu ikiwemo ya
vijana, msiwasahau wananchi, jiwekeeni utaratibu wa kuwatembelea ili
mfahamu kero zao, msidhani mikutano ya mbunge pekee ndiyo njia ya
kusikiliza na kutatua kero za wananchi,” alisema.
Aliwataka
viongozi hao kamwe wasibweteke wala kusuasua katika kufanya mikutano na
kutembelea wananchi, ambao kimsingi ndio wanaowatumikia.
“Ndiyo
maana tumewapa baiskeli makatibu watendaji wa Chama na UVCCM wa kila
Kata ili ziwasaidie kuwafikia wananchi na wanachama kwa wakati muafaka,
nao wana wajibu wa kuwatembelea wananchi na kukiimarisha Chama,” alisema
Dk. Kamani.
Hivi
karibuni, Mwenyekiti huyo wa Chama wa mkoa wa Simiyu alitoa baiskeli 39
zenye thamani ya zaidi ya sh. milioni 5.8 kwa wenyeviti na makatibu
Kata wa CCM na Makatibu wa UVCCM kwa ajili ya kuwasaidia usafiri wa
kuwafikia wanachama na wananchi kwa urahisi.
Awali,
mwishoni mwa wiki, Dk Kamani alitembelea na kukagua ujenzi wa wodi ya
Wazazi unaendelea katika Zahanati ya Kata ya Lamadi Kijijini Lukungu,
inayojengwa kwa thamani ya sh. milioni 75 zilizotolewa na AMREF mkoani
Simiyu, chini ya kampeni ya Uzazi-Uzima.
Mbunge
wa Jimbo la Busega, ambaye pia ni Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na
Uvuvi, Dk. Titus Kamani, akishuhudia maji yakitiririka baada ya
kukamilika kwa mradi wa maji wa Kijiji cha Manala Kata ya Badugu
wilayani Busega. Kulia ni Katibu wa CCM wa Wilaya ya Busega, Agatha
Magonela.
Dk. Titus Kamani, akimtwisha ndoo ya maji mama mmoja mkazi wa Kijiji cha Manala, baada ya kufungua mradi huo.
Dk.
Kamani akikagua msingi wa Kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino)
kinachojegwa katika Kijiji cha Lukungu Lamadi wilayani humo, mbele yake
ni Mratibu wa kituo hicho, Mudy Gimonge.
Dk.
Kamani akishiriki na baadhi ya wananchi wa Lukungu kusomba tofali za
ujenzi wa kituo cha kulelea walemavu wa ngozi (albino).
No comments:
Post a Comment