Rais
Jakaya Mrisho Kikwete na Mama Salma Kikwete pamoja na viongozi wa serikali wakiwepo Waziri
wa Ardhi na maendeleo ya Makazi, Waziri wa Nishati na
Madini, Waziri wa Ujenzi wakiwa wameshika utepe tayari kwa Rais kuukata na
kuelekea kubonyeza kitufe ikiwa ni ishara ya uzinduzi wa mradi huo wa umeme.
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe
kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Rais akifunua kitambaa mahali palipowekwa kitufe
kwa ajili ya uzinduzi rasmi
Na Mwandishi Wetu
Rais
wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dk. Jakaya Mrisho Kikwete
amezindua mradi wa kusambaza umeme vijijini unaosimamiwa na Wakala wa
Umeme Vijijini (REA) utakaowanufaisha wakazi wa Mkoa wa Ruvuma
utakaochangia kuongeza kasi ya maendeleo vijijini.
Rais
Jakaya Kikwete yuko katika ziara yake ya kikazi ya kukagua miradi ya
maendeleo katika mkoa huo lengo likiwa ni kutimiza azma ya serikali ya
kuwa kila mwananchi anapata huduma ya nishati ya umeme.
Kwa
upande wake Waziri wa Nishati na Madini, Prof. Sospeter Muhongo
amewahakikishia wakazi hao kwamba hadi ifikapo mwezi Novemba mwaka huu
vijiji vyote vilivyoko katika mradi wa kusambaza umeme vijijini awamu ya
II watakuwa tayari wanatumia nishati hiyo kwa wale watakao wamemudu
gharama ya Shilingi Elfu Ishirini na Saba ya kuunganishiwa nishati
hiyo.
Imeelezwa
kwamba mradi wa usambazaji wa umeme vijijini katika mkoa wa Ruvuma
utagharimu kiasi cha Tsh. 26.53 bilioni zitakazohusisha ujenzi wa njia
za umeme zenye msongo wa kilovolti 33 zenye jumla ya urefu wa km 538,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovolti 11 yenye urefu wa km 23,
ujenzi wa njia ya umeme msongo wa kilovoti 0.4 yenye urefu wa km 272,
ufungaji wa transfoma 129 za ukubwa mbalimbali pamoja na kuunganisha
wateja 7,488.
Mradi
huu utatekelezwa na kampuni ya Lanka Transfomers Limited, (LTL) ya
nchini SRILANKA kwa mkoa wa Ruvuma. Mradi huo unatarajiwa kukamilika
ifikapo Juni 2015 na kunufaisha wakazi wa wilaya za Songea, Tunduru,
Mbinga na Nyasa.
Pamoja
na uwepo wa mradi huo pia kuna mradi wa kuongeza nguvu ya umeme kwenye
wilaya za Mbinga na Tunduru unaotekelezwa na kampuni ya Taikai Co.Ltd
ambapo tayari amekamilisha survey ya vituo vyote na ameshawasilisha
transifoma ya kituo cha Tunduru.
Prof. MUHONGO amesema mradi wa kuongeza nguvu ya umeme utagharimu kiasi
cha pesa za kitanzania Shilingi bilioni 2.27 zitakazohusisha ujenzi wa
vituo viwili vya kuongeza nguvu ya umeme kutoka kilovoti 11 hadi kufikia
kilovoti 33 kwa ajili ya kufikisha umeme katika vijiji vilivyoko
mbali.
Vituo
hivyo vitakuwa na transifoma zenye uwezo wa kilowati 3,000 (3.0MW) kila
kimoja.
Kwa upande wake Mbunge wa MBAMBABAY Captain JOHN KOMBA ameishukuru
serikali ya Chama Cha Mapinduzi (CCM) kwa kutekeleza ilani ya uchaguzi
ya chama hicho ikiwa ni pamoja na kuboresha miundombinu ya barabara hasa
madaraja, kuwawekea umeme, na kupandishwa hadhi kituo cha afya na kuwa
hospitali ya wilaya.
Miradi
ya REA awamu ya II imeanza kutekelezwa rasmi Novemba 2013 na inatakiwa
kukamilika ifikapo Juni2015 kwa nchi nzima hivyo kuchangia katika
kuongeza kiasi cha wananchi waliofikiwa na huduma ya umeme kufikia
asilimia 30.
No comments:
Post a Comment