Diwani wa kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa John Kiowi kulia akiwa amevalia sare za CCM huku akieleza imani yake kwa mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe katika kuwatumikia wananchi wa jimbo la Ludewa na kudai kuwa yeye si mpinzani kama wengine , kushoto ni mbunge Filikunjombe akimsikiliza kwa makini wakati wa shughuli ya maendeleo ya kuchimba mashimo ya nguzo za umeme kwenda Lupingu. |
|
Mbunge Filikunjombe shimoni na diwani wa TLP wakishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme. |
Mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe akishiriki kuchimba mashimo ya nguzo za umeme pamoja na wananchi wa kata ya Lupingu |
Na Francis Godwin Blog
DIWANI wa chama cha Tanzania
Labour Party (TLP) kata ya Lupingu wilaya ya Ludewa mkoani Njombe
John Kiowi amempongeza mbunge wa jimbo la Ludewa Deo Filikunjombe kwa
jitihada zake anazozifanya katika kuwapelekea maendeleo wananchi wa
Ludewa huku akiwashangaa wapinzani wanaopinga jitihada mbali mbali
zinazofanywa na serikali ya chama cha Mapinduzi (CCM) na kudai
kuwa yeye si mpinzani wa uchwara wa kupinga maendeleo .
Akizungumza
na wanahabari jana wakati wa zoezi la mbunge Filikunjombe na
diwani huyo kushiriki na wananchi wa kata ya Lupingu kuchimba
mashimo ya nguzo za umeme na kusimika nguzo hizo za umeme , Kiowi
alisema kuwa ni zaidi ya wabunge watano wamepata kuliongoza
jimbo hilo la Ludewa ila ni mara yake ya kwanza kuona mbunge
akishiriki bega kwa bega na wananchi wake kuchimba mashimo kama
ambavyo mbunge huyo anafanya .
"
Jamani wananchi kwanza ni jambo la kumpongeza mbunge wetu mbali ya
kuhimiza wananchi ila mwenyewe pia amekuwa mstali wa mbele katika
kushiriki tofauti na wana siasa wengine ambao muda wote wao ni watu
wa majukwaani ila vitendo sifuri .....nasema Ludewa imempata mbunge
na niweke wazi hapa mimi sio mpinzani hivi tujiulize wenyewe
nikisema mimi ni mpinzani napinga nini hapa haya maendeleo ni kwa
faida yangu na wananchi wote sasa kama mbunge wa CCM wanafanya kuna
haja ya upinzani hapa "
Kiowi
alisema kuwa ataendelea kufanya kazi na mbunge Filikunjombe ikiwa ni
pamoja na kusimamia utekelezaji wa ilani ya CCM katika kata yake kwani
chama chake cha TLP katika kata ya Lupingu kinatekeleza ilani ya
CCM ambacho ndicho chama kilichopo madarakani na peke yake bila
kumtegemea mbunge hawezi kufanya lolote.
Diwani
Kiowi ambae alikuwa amevalia sare za CCM katika shughuli hiyo ya
maendeleo alisema kuwa katika kuhakikisha kuwa yeye si mpinzani ila
ni mpenda maendeleo hata sare za CCM zinazotolewa na mbunge
Filikunjombe amekuwa akizivaa na amekuwa mstali wa mbele kumpongeza
mbunge huyo kutokana na kuwa mbunge wa mfano kwa kufanya kazi bila na
makundi yote .
Hata
hivyo diwani huyo alisema kuwa katika suala la maendeleo hata kuwa
tayari kuona watu wachache wakimkwamisha mbunge huyo kwa kushindwa
kuunga mkono jitihada zake katika kuwaletea maendeleo na kudai kuwa
kwa upande wake anaona wapinzani ni wana CCM wenyewe wasiopenda
kujivunia maendeleo makubwa mbayo mbunge Filikunjombe ameyapeleka
Ludewa .
Kwa
upande wake mbunge Filikunjombe mbali ya kumpongeza diwani huyo wa
TLP kwa kushiriki vema katika shughuli za maendeleo bado alisema
kuwa ni wapinzani wachache nchini ambao wanajitoa kama diwani huyo
katika shughuli za maendeleo zinazoitishwa na mbunge wa CCM
Alisema
yapo baadhi ya maeneo wabunge ama madiwani wa upinzani wamekuwa ni
watu wa kupinga kila jambo linalofanywa na mbunge ama diwani wa CCM
na wengine wasiokuwa na uzalendo na Taifa wamefikia hatua ya kubeza
hata jitihada zinazofanywa na Rais Dr Jakaya Kikwete katika kuliletea
maendeleo Taifa jambo ambalo si la kizalendo hata kidogo na kuwa huo
si upinzani wa kweli.
"
Nataka kusema hivi wakati wa kampeni ndio wakati wa kupingana
kisera ila baada ya chaguzi hakuna haja ya kuendelea kupingana ni
kuwa wamoja na kuwaletea wananchi maendeleo hivi hebu niulize ujenzi
huu wa barabara ya Lupingu ,Ludewa na Njombe Ludewa unaoendelea ni
kwa faida ya nani hii barabara inatumiwa na wana CCM pekee mbona
hata wapinzani mnapita katika barabara hiyo hiyo sasa unapinga nini
wakati huu wa CCM kutekeleza ilani yake ....tuwe na uzalendo wa
nchi yetu tusiwe wa kupinga kila kitu na mimi nikueleze wazi kama
ungejaribu kupinga mradi huu wa umeme kwa kutoshiriki tungeonana
wabaya mbele ya safari"
Akielezea
mradi huo wa umeme Filikunjombe alisema kuwa kwa kasi ambayo
wananchi wanaenda nayo katika kujitolea nguvu zao kuchimba mashimo
na kusogeza nguzo katika mashimo hayo ni wazi mradi huo wa umeme
utakamilika kabla ya Desemba mwaka huu .
Aidha
alisema kuwa wakati akiingia madarakani mwaka 2010 ni kijiji kimoja
pekee cha jimbo hilo la Ludewa ambacho kilikuwa na umeme wa mafuta
ila sasa zaidi ya vijiji 10 vina umeme na kuwa hadi sasa jumla ya
vijiji 49 vitafikiwa na mradi wa umeme huo ambao unatekelezwa kwa nguvu
za serikali ya Tanzania , Swedeni na kanisa na Romani Katoliki
Dayosisi ya Njombe.
|
No comments:
Post a Comment