Mkurugenzi
wa Amref Health Africa Tanzania Dr. Festus Ilako (wa kwanza Kushoto)
Akimkaribisha Waziri wa Afya Dr. Seleman Seif Rashid kuzindua Nembo
Mpya.
Waziri
wa Afya, Mwenyekiti wa bodi ya kimataifa ya Amref Health Africa Mr.
Omari Issa, Dr. Festus Ilako na wafanyakazi wa Amref Health Africa
Tanzania katika picha ya pamoja baada ya Uzinduzi.
wadau na wageni waalikwa katika uzinduzi huo
Picha ya pamoja ya meza kuu na wadau wa Amref Health Africa baada ya Uzinduzi.
*****************************************
SHIRIKA
la kimataifa lisilokuwa la kiserikali la Afrika Medical and Research
Foundation (Amref) limezindua rasmi jina na nembo yake mpya ambapo sasa
litajulikana kama Amref Health Africa Tanzania.
Uzinduzi
huo ulifanywa jijini Dar es Salaam Ijumaa ya tarehe 4/7/2014 na Waziri
wa Afya na Ustawi wa Jamii, Dk. Seif Rashid ambapo Mkurugenzi Mkazi wa
Amref Health Africa Tanzania, Dk. Festus Ilako, alisema imebidi kubadili
jina na nembo yao ili kuendana na majukumu yao ya sasa ambayo yamekuwa
ni zaidi ya utafiti na utoaji wa huduma za tiba.
“Kwa
sasa tunajikita pia katika uimarishaji wa mifumo ya utoaji wa huduma za
afya, mafunzo, mikakati ya utoaji wa huduma/miradi ya afya ya mama na
mtoto, ukimwi, kifua kikuu, malaria, huduma za madaktari bingwa na
maabara.
“Mabadiliko
ya jina na nembo yetu hayataathiri aina ya walengwa wetu wakuu;
tutaendelea kufanya kazi kwa karibu kabisa,” alisema Dk. Ilako.
Alitoa
mfano kuwa kila siku wanawake 22 wanapoteza maisha nchini wakati wa
kujifungua na kwamba mpango wa Amref ni kupunguza vifo hivyo.
Waziri
Seif katika hotuba yake ya uzinduzi, alisema serikali inatambua mchango
mkubwa wa taasisi hiyo na kwamba wamesaidia kupunguza maambukizi ya
virusi vya ukimwi (VVU) kutoka kwa mama kwenda kwa mtoto, mimba za
utotoni na upatikanaji wa majisafi na salama.
No comments:
Post a Comment