Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk.
Mary Nagu akihutubia wakati wa ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu
Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Mh. Nagu katika hotuba
yake,amesema atawasimamia Makatibu hao na kuhakikisha wanaanzisha Benki
yao ambayo itawawezesha kuweka abiba zao na kukopeshana pia.
Mgeni
Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa
Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki akitoa hotuba yake katika ufunguzi
wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013
jijini Mwanza.Mh. Kairuki amewahimiza Makatibu Muhtasi hao kuhakikisha
wanaudumisha na kuulinda umoja walionao,kwani umoja ndio msingi wa
maendeo.
Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda akiteta jambo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu pamoja na Mgeni Rasmi katika Kongamano la Makatibu Muhtasi Tanzania,Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki wakati wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.
Picha ya pamoja.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu - Uwekezaji na Uwezeshaji ambaye pia ni Mlezi wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania (TAPSEA),Mh. Dk. Mary Nagu akifurahi jambo na Naibu Waziri wa Katiba na Sheria,Mh. Angela Kairuki mara baada ya ufunguzi wa Kongamano la nne la Makatibu Muhtasi Tanzania,leo Julai 11,2013 jijini Mwanza.Kushoto ni Mwenyekiti wa Chama cha Makatibu Muhtasi Tanzania,Bi. Pilli Mpenda. Picha na Othman Michuzi.
No comments:
Post a Comment