MAISHA NA UJASIRIAMALI : FAIDIKA YAWAWEZESHA WAJASIRIAMALI BAADA YA MAFUNZO YA BIASHARA - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633


PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0676 643 633

Friday, 18 July 2014

MAISHA NA UJASIRIAMALI : FAIDIKA YAWAWEZESHA WAJASIRIAMALI BAADA YA MAFUNZO YA BIASHARA


 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akizungumuza na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Katikati ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bi. Joan Kitembe kutoka Mkoa wa Arusha, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bi. Bahati Bukubilo kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa kanza kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bw. Linus Mwangoya kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa pili kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
 Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi akimkabidhi zawadi Bw. Bakari Khamisi kutoka Mbeya, baada ya kuibuka mshindi wa tatu kimkoa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara ulioandaliwa na taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Wapili kushato ni Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore (wa nane kulia kwa waliosimama) pamoja na Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi (kushoto kwa Marion) wakiwa katika picha ya pamoja na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA.
Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore akizungumuza na wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam waliopata mafunzo juu ya uendeshaji biashara, kabla ya kupata fedha kwa ajili ya mitaji kutoka taasisi ya kifedha ya FAIDIKA. Kushoto ni Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi na kulia ni Mwalimu wa wajasiriamali Bi. Mariam Tambwe

Taasisi ya kifedha ya FAIDIKA, inayoshughulika na utoaji mikopo hapa nchini, imewawezesha wajasiriamali kutoka mikoa ya Mbeya, Arusha na Dar es Salaam baada ya kuwapa mafunzo ya njia bora ya ufanyaji biashara. 

Wajasiriamali hao ni miongoni mwa wale 300 waliopata mafunzo na baadae kuingizwa katika mashindano ya kuandika mchanganuo wa biashara, kisha kuwapata washindi watatu katika kila mkoa. 

Akizungumuzia mashindano hayo, Ofisa Mtendaji Mkuu wa FAIDIKA Marion Moore alisema washindi watano katika kila mkoa walipatikana baada ya kuwasilisha maandiko ya mchanganuo wa biashara ambazo zilionekana kukidhi vigezo vilivyowekwa na walimu wa wajasiriamali hao.

“Leo FAIDIKA inatimiza ahadi yake ya kuwapa wajasiriamali ambao michanganuo yao ya biashara imeonekana kuwa bora zaidi. Katika kila mkoa, mshindi wa kwanza amepata Tsh milioni 1.2, mshindi wa pili Tsh 800,000, watatu 500,000, wanne Tsh 300,000 na wa tano kupata 200,000.

“FAIDIKA ilifanya mashindano haya baada ya mafunzo kwa wajasiriamali zaidi ya 300 kutoka katika mkoa wa Dar es Salaam, Mbeya na Arusha, ikilenga jumla ya makundi matatu: Wanawake wa Tanzania asilimia 34, watu wenye ulemavu asilimia 32 na watu wa kawaida mitaani asilimia 34," alisema.

Awali, mgeni rasmi katika hafla hiyo ya utoaji zawadi kwa washindi, iliyofanyika Jijini Dar es Salaam jana, Mkurugenzi wa viwanda vidogo na biashara ndogo ndogo na za kati kutoka Wizara ya Viwanda na Biashara, Consolata Ishebabi aliwataka wafanyabiashara ndogo ndogo kurasimisha biashara zao ili kuepuka usumbufu wanaopata wa kupoteza mali zao na mitaji ya biashara wakati wa oparesheni ya safisha mji.

Bi. Ishebabi alisema biashara zilizorasimishwa na kupewa leseni, hupangiwa utaratibu mzuri wa kufanyia shughuli za biashara, hivyo kumfanya mjasiriamali awe na nafasi ya kutumia biashara yake kukopa mikopo katika taasisi mbali mAbali za kifedha.

“Wafanyabiashara ndogo ndogo wakijisajili katika mfumo rasmi, inakuwa rahisi hata kwa taasisi zinazotoa mikopo kuwaamini na kuwapa mikopo na kuweza kutanua mitaji yao. Bila kuwa rasmi, ni vigumu kuaminika. Kwa biashara zilizorasimishwa, oparesheni ya safisha mji haiwaathiri kwani watakuwa katika maeneo maalum waliopangiwa kufanya shughuli zao,” alisema Bi. Ishebabi.

Alipongeza uongozi wa FAIDIKA kwa kuja na utaratibu wa kuwafuatilia wajasiriamali ili kuhakikisha kuwa wanazingatia biashara walizoombea hela na kuwaonyesha njia bora ya kuboresha biashara zao, na kuzitaka taasisi zingine zinazotoa mikopo kuiga mfano huo, mbali na kujali tu kama mkopaji anarejesha mkopo.

No comments:

Post a Comment