Timu ya Uholanzi imeibamiza Timu ya Brazil Kwa jumla ya mabao 3 Kwa 1 , katika kinyang'anyiro cha kumtafuta mshindi wa Tatu katika kombe la Dunia 2014.
Hivyo , Uholanzi imeshika nafasi ya Tatu na Brazil kutoka mshindi wa NNE.
Fainali , Zitachezwa baadae kati ya timu ya Ujerumani na Argentina ...Tusubiri tupate mshindi...au unaweza kutabiri mshindi hapa
Uholanzi
ilimaliza katika nafasi ya tatu katika kombe la dunia huko Brazil baada
ya kuchomeka msumari wa moto ndani ya kidonda cha wenyeji walipowalaza
mabao 3-0 mjini Brasilia siku ya jumamosi.
Mashabi
wa Brazil waliwazomea wachezaji wao akiwemo kocha Luiz felipe Scolari
kwa utendakazi duni katika mechi hizi mbili za mwisho Brazil ilipofungwa
mabao 10 nayo ikifunga moja.
Brazil
ilifungua mechi hii kwa kasi lakini ikafungwa bao la kwanza kunako
dakika ya pili ya mechi hiyo kupitia kwa mkwaju wa penalti uliopigwa na
Robin va Persie.
Nahodha
Thiago Silva alimtega Arjen Robben nje ya eneo lakini refarii kutoka
Algerian Djamel Haimoudi akaamua kumwadhibu kwa kadi ya njano na penalti
dakika mbili tu baada ya mechi hiyo kuanza badala ya kumwonesha kadi
nyekundu .
Mashambulizi
ya Uholanzi yalizaa matunda kunako dakika ya 15 ya mechi hiyo David
Luiz alipookoa mkwaju uliokuwa unaelkea wavuni kwa kichwa lakini
ukamwangukia Daley Blind naye akaurejesha humohumo .
Kila
mtu uwanjani alifurahia Brazil walipofanya mashambulizi kwenye lango la
Uholanzi lakini kila mara walipofika katika eneo walikosa makali na
kushindwa kupenyeza safu ya ulinzi ya Uholanzi.
Uholanzi
walisalia kulinda ngome yao na kila walipopata fursa walitekeleza
mashambulizi kwa lango la Selecao ambao walionekana imara tofauti kabisa
na timu iliyodenguliwa 7-1 na Ujerumani juma lililopita huko Belo
Horizonte.
Hata
hivyo Georginio Wijnaldum aliifungia Uholanzi bao la tatu kwa nunge na
kumpa kocha Louis va Gaal kwaheri na nishani ya shaba kutoka kwa fifa.
Kwa upande wake Scolari alisalia na maswali mengi bila majibu baada ya safu yake ya ulinzi kuvuja mabao 10 katika mechi mbili.
Bila
shaka atakuwa na kibarua kigumu akijaribu kuiokoa kibarua chake kisiote
nyasi punde baada ya kipenga cha mwisho cha kombe la dunia huko Maracana
jumapili julai tarehe 13 .Chanzo BBC Swahili
No comments:
Post a Comment