HILI NALO JIPYA : KONOKONO WAKAMATWA MAREKANI - Wazalendo 25 Blog

Glory to Story.

Habari Mpya

PRINTING / GRAPHICS / DESIGN : 0784 643 633

Tuesday, 15 July 2014

HILI NALO JIPYA : KONOKONO WAKAMATWA MAREKANI

Konokono sitini na saba walio hai wamekamatwa na maafisa wa forodha wa Marekani.
Konokono hao ambao hawaruhusiwi kuingizwa Marekani walikamatwa na maafisa wa forodha kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Los Angeles.
Walikuwa wamesafirishwa kutoka Nigeria, wakipelekwa kwa mtu mmoja mjini California, amesema Lee Harty, msemaji wa mamlaka ya forodha.
Konokono hao ni miongoni mwa konokono wakubwa duniani na huweza kukua na kufikia urefu wa sentimita 20, wamesema maafisa.
Idara ya kilimo ya Marekani imewateketeza konokono hao baada ya kuwakagua, amesema Bi Harty, kwa sababu hubeba wadudu ambao ni hatari kwa binaadam, wakiwemo wadudu wanaosababisha homa ya uti wa mgongo. Chanzo: Salim Kikeke

No comments:

Post a Comment