Meneja
wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John akizungumza na wahariri
walipotembelea mradi wa nyumba za makazi za Shangani Mjini Mtwara leo
jioni. Kutoka Kulia ni Theophi Makunga, Mhariri na Meneja Bishara wa
Mwananchi Communications Limited, Jesse Kwayu Mhariri Mtendaji wa
Nipashe na Bakari Machumu Mhariri Mtendaji wa Mwananchi Communications
Limited. (Picha zote kwa hisani ya Shirika la Nyumba la Taifa)
Wahariri
wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba
la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa
fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Wahariri
wakifuatilia maelezo ya Meneja wa mkoa wa Mtwara wa Shirika la Nyumba
la Taifa, Joseph John (hayupo pichani) wakati Meneja huyo akitoa taarifa
fupi ya utekelezaji wa mradi huo jana mbele ya Wahariri.
Wahariri
wa vyombo mbalimbali vya habari nchini wakimsikiliza Meneja wa Shirika
la Nyumba Mtwara, Joseph John walipotembelea mradi wa nyumba za makazi
za Shangani Mjini Mtwara jana jioni. Kutoka kulia ni Jabir Idrisa,
Mhariri wa Mwanahalisi, Salim Salim nguli wa Habari na Mwalimu kutoka
Zanzibar, Joseph Kulangwa wa Uhuru Publications.
Mojawapo
ya majengo ya majengo ya Mradi wa nyumba za makazi za Shangani kama
linavyoonekana leo hii. Ni mojawapo kati ya majengo matatu yenye nyumba
10 kila moja na hivyo kufanya idadi kufikia 30.
Meneja
wa Shirika la Nyumba Mtwara, Joseph John akiwa pamoja na Meneja
Mawasiliano wa Shirika la Nyumba la Taifa , Yahya Charahani kwenye Mradi
wa nyumba za makazi Shangani
Juzi,
Alhamisi (Julai 10, 2014) na jana Ijumaa (Julai 11, 2014) jopo la
Jukwaa la wahariri takriban 85 walitembelea kwenye miradi yetu miwili,
mmoja wa ujenzi wa nyumba za gharama nafuu Mtanda mkoani Lindi na
mwingine wa nyumba za makazi za kati na juu zilizopo eneo la Shangani
Mtwara.
Jopo
hilo likiongozwa na Mwenyekiti wa Jukwaa hilo, Absalom Kibanda na
Katibu wa Jukwaa hilo, Neville Meena. Walisomewa taarifa fupi ya
maendeleo ya ujenzi wa miradi ya Nyumba hizo zipatazo 30 Lindi ambazo
sasa zimefikia kwenye hatua za mwisho tayari kwa kukabidhiwa kwa
wamiliki wake kwani nyumba zote 30 tayari zilishanunuliwa na zile za
Mtwara ambazo pia ni 30, 10 kati ya hizo zikiwa zimeshanunuliwa.
Miongoni
mwa mambo makubwa yaliyozungumzwa na wahariri hao ni kuliomba kuendelea
kusimamia azam yake ya kuwauzia nyumba Watanzania wa kipato cha chini,
kwani kwa kufanya hivyo watanzania wa kawaida watakuwa na uwezo wa
kumiliki nyumba na siyo kuendelea kuwa wapangaji wa shirika.
No comments:
Post a Comment